10/05/2013
Anaitwa ALESSANDRA CORINE AMBROSIO
Ni MODEL wa ki'Brazil, alizaliwa katika manispaa ya ERECHIM nchini BRAZIL april 11, 1981, wazazi wake ni wa asili ya ITALY wenye uraia wa BRAZIL ambao ni wafanya biashara wanaomiliki petrol station nchini humo
Akiwa na umri wa miaka 12 AMBROSIO alijiunga na mafunzo ya MODELLING, na mnamo mwaka 1996 alishiriki shindano la taifa lililojulikana k**a ELITE MODEL LOOK ambapo alifanikiwa kuingia 20 bora.
Siku zote ktk makuzi yake AMBROSIO hakupendezwa kabisa na masikio yake yaliyokuwa makubwa aliyohisi yanaweza kuwa tatizo katika fani yake hivyo alipofikisha umri wa miaka 11 aliamua kufanyiwa plastic surgery kupunguza ukubwa wa masikio hayo hali iliyokuja kumtesa miaka miwili mbeleni kwani aliugua vibaya mno, hali aliyokuja kuizungumzia mwaka 2006 ktk kipindi cha THE TYRA BANKS SHOW kuwa hatothubutu tena kuja kufanyiwa plastic surgery maishani mwake.
Safari ya MODELLING kwa AMBROSIO ilianza pale tu alipojiunga na mafunzo na baadae kujiunga na DILSON STEIN MODELLING AGENCY akiwa na umri wa miaka 15, baadae kushiriki shindano la ELITE MODEL LOOK.
DILI KUBWA na la kwanza kulifanya ni lile la kutokea kwenye cover la magazine kubwa nchini BRAZIL ya ELLE MAGAZINE, ELLE walizitambulisha baadhi ya picha za AMBROSIO ktk kampuni ya mavazi ya GUESS iliyopo nchini marekani akafanikiwa kusaign dili kwenye kampuni hiyoiliyompa mashavu mengine ya kutokelezea kwenye matangazo mbalimbali k**a REVLON, CHRISTIAN DIOR, GIORGIO ARMANI, RALPH LAUREN na vilevile kwenye calenda mbalimbali k**a PIRELLI
Tangu hapo ndipo alipoanza ku'shine. Kwa kufanya CATWALKS kwa madesigner mbalimbali wakubwa k**a PRADA, CHANEL na OSCAR DE LA RENTA, pia ametokelezea mbalimbali za kimataifa k**a COSMOPOLITAN, ELLE, GQ, HARPER's BAZAAR, MARIE CLAIRE, OCEAN DRIVE, VOGUE na akiwa ni MODEL pekee aliyetokea kwenye cover la GLAMOUR mwaka 2006.
Mwaka 2004 AMBROSIO alizindua vazi lake la kuogelea alilolipa jina lake ALESSANDRA AMBROSIO alilofanikiwa kuuza units 10,000 ndani ya mwezi wa kwanza tangu kuzinduliwa
AMBROSIO alifanikiwa kusiniwa k**a kisura kwenye kampuni ya NEXT ya uingereza na ku'STAR kwenye kampeni ya TV kwa muda wa miaka 12.
AMBROSIO alitajwa na mtandao wa FORBES kushika nafasi ya 5 kwenye list ya MODELS wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi duniani kwa kukadiliwa kuwa alifanikiwa kuingiza kiasi cha dola za kimarekani million 5 kwa mwaka 2010-2011.
Octoba 2011 AMBROSIO alichaguliwa kuwa blogger wa kampuni ya VOGUE kwa kucomment nguo zake na kupost picha yake moja kila siku kwa mwezi mmoja.......Ewe MODEL wa Tanzania linashindikana lipi kwako kufikia hatua aliyonayo AMBROSIO, usiangalie uko nchi gani, familia yako inauwezo kiasi gani, elimu yako ni ya kiwango gani , kwani mwisho wa yote hayo si kitu ukiamua kujituma, sisi tunaamini kwa nguvu kabisa kuwa JUHUDI ZA KWELI, DAIMA SI TASA!!!!.