03/06/2026
KWA NINI JUPITER HUITWA FAILED STAR
Watu wengi hudhani kwamba Jupiter huitwa Failed Star kwa sababu ya ukubwa wake, Sayari hii ndiyo kitu cha pili kwa ukubwa kwenye mfumo wa Jua baada ya Jua kwenye mfumo huu.
Lakini ili kitu kiwe Nyota hatuangalii tu Ukubwa, bali sifa za kuifanya iwe na uwezo wa kuunda,mwanga, joto lake yenyewe.
Jupiter sio tu kuwa kubwa, dani yake kuna mazingira ya kutisha kuliko imagination nyingi za science fiction.
Ilikosa kidogo tu kuwa Nyota.
Jupiter ni Gas Giant. Haina ardhi ngumu ya kusimama k**a Dunia.
Sehemu kubwa imeundwa na Hydrogen na Helium, gesi zile zile zinazounda Jua au Nyota yeyote.
Kwa hiyo baadhi ya watafiti huiita โfailed starโ kwa sababu ilibaki kidogo kuwa nyota, kwa sababu mass yake haikutosha kuunda nuclear fusion.
Ukijaribu kushuka ndani ya Jupiter, usingetua popote. Hakuna ardhi ni mawingu tu ya Hydrogen na Helium. Pressure ingeongezeka taratibu unaposhuka chini mpaka mwili wako usagwe kabisa.
Kadri unavyozama ndani zaidi, Hydrogen inaanza kubadilika kuwa kitu cha ajabu kinachoitwa Metallic Hydrogen.
Hii ni Hydrogen iliyobanwa kwa pressure kubwa sana mpaka inaanza ku-behave k**a chuma kinachopitisha umeme.
Na hapo ndipo siri ya nguvu nyingine ya Jupiter inaanza. Inaanza kuunda Magnetic field.
Magnetic field ya Jupiter ni kubwa na yenye nguvu ya kutisha sana. Inaaminika kuwa na nguvu zaidi ya mara 10 mpaka 20 ya magnetic field ya Dunia.
Ukisimama karibu na Jupiter bila protection, radiation yake inaweza kukuua ndani ya muda mfupi.
Magnetosphere yake ni kubwa kiasi kwamba k**a macho ya binadamu yangeweza kuiona kutoka Duniani, ingeonekana angani ikiwa kubwa kuliko Mwezi.
Yaani, Jupiter si inaonekana k**a kidot kidogo cha mwanga kinawaka usiku k**a nyota, sasa k**a ukanda wake wa magnetosphere ungeonekana umeizingira, kwa pamoja vingeonekana k**a ukubwa wa mwezi.
Magnetosphere ni eneo kubwa la invisible energy za magnetic Field na umeme, linalozunguka sayari hiyo na kushika chembechembe za radiation kwa nguvu kubwa sana.
Na ndani ya mazingira hayo ndipo kuna dhoruba kubwa zaidi kati ya zote kwenye mfumo wa Jua.
The Great Red Spot.
Hii ni storm kubwa inayozunguka kwenye atmosphere ya Jupiter kwa zaidi ya miaka 300 ambayo binadamu wamekuwa wakiiona tangu ilipongundukiwa na Galileo Galilee miaka ya 1600.
Upepo wake unaweza kuzidi kilomita 600 kwa saa. Na ukubwa wake ni mkubwa kiasi kwamba Dunia nzima inaweza kutoshea ndani yake.
Fikiria kimbunga kikubwa kuliko sayari yetu kikizunguka bila kusimama kwa karne tatu.
Na bado Jupiter haijaacha kushangaza.
Ina miezi zaidi ya 90 inayojulikana mpaka sasa. Ni k**a ina mfumo wake wa sayari zinazoizunguka. Baadhi yake ni dunia za ajabu zenye bahari zilizofichwa chini ya barafu.
Mwezi wa Europa unaaminika kuwa na bahari kubwa chini ya uso wake wa barafu. Bahari hiyo inaweza kuwa na maji mengi kuliko bahari zote Duniani zikiunganishwa pamoja.
Ndiyo maana Jupiter imekuwa moja ya maeneo muhimu sana kwenye utafiti wa maisha ya nje ya Dunia.
Lakini pamoja na maajabu yake yote, bado haijaweza kuwa Nyota k**a ilivyo Jua.
Inaitwa Failed Star kwa sababu ya kukosa uzito wa kutosha kusababisha zile Hydrogen bonding za kulipuka kuunda joto na mionzi.
Mgandamizo uliopo kwenye Jupiter unasababisha Hydrogen kuwa metal ngumu inayopitsha umeme, lakini k**a mgandamizo huu ungeongezeka walau kufika mara 10 ya mgandamizo wa sasa, hapo Hydrogen ingewza kuungana kuunda Helium.
Na hapo ndipo ingeweza kufanya Thermonuclear Fusion kuunda Joto, Mwanga n mionzi k**a zinavyofanya Nyota nyingine.
Kwa mgandamizo kuongezeka mara 10, inahitaji uzito wake kuongezeka mara 100, k**a uzito ungeongezeka kiwango hicho basi Jupiter inakuwa Nyota inayowaka mwanga wake yenyewe na kumiliki mfumo wake unaojitegemea.
Hata hiyo mpaka sasa, licha ya kushindwa kuwaka moto, bado Jupiter ina mvumo wa miezi kidhaa inayozunguka, ikiwa na gravity kushinda sayari zote kwenye mfumo wa Jua pia imeundwa na gesi za Hydrogen na Helium kwa wingi. Ni Gas giant isiyolinganishwa na chochote kwenye mfumo wa Jua.
Mimi ni Ommy Mkaly Official nikikudadavulia hizi sayansi Ngumu kwa lugha nyepesi