Ovie Together, We smile.

02/01/2025

Tufanye mazoezi aisee 🏋️🏋️ 🏋️ hizi dharau Sasa!!!

02/01/2025

Tufanye mazoezi aisee 🏋️🏋️🏋️

RIWAYA: WAKILI WA KUJITEGEA.MWANDISHI: Octa PK.UMRI: +18.Mawasiliano: +255624102400.Whatsapp:. +255624102400.*****SEHEMU...
11/06/2021

RIWAYA: WAKILI WA KUJITEGEA.
MWANDISHI: Octa PK.
UMRI: +18.
Mawasiliano: +255624102400.
Whatsapp:. +255624102400.

*****SEHEMU YA KWANZA*****
Majira ya saa saba alasiri, siku ya jumatano ya tarehe 09/03/2020 ilikika sauti ya hakimu mkazi wa mahak**a ya kisutu ikimhukumu mwandishi wa habari wa kituo cha habari cha UTV(Universal Television). Kwa amri ya mahak**a mwandishi huyo alihukumiwa kwenda jera kwa kifungo cha maisha akituhumiwa kumuua mkewe Bi. Mery Sayuni kwa kumnyonga hata kifo.
Sauti kali ya maumivu ya moyo ilimtoka Bw. Nandrie Kweka kwa maamuzi yaliyotolea na mahak**a hiyo. Kila aliyekuwa ndani ya mahak**a hiyo alifurahi kwa maamuzi ya mahak**a hiyo na kilio chake kilionekana si chochote mbele ya umati uliokuwa ndani ya mahak**a hiyo. “Ghafla!” aliacha kulia na kuanza kucheka kwa nguvu huku akinyoosha mikono kwa askari aliyekuwa mbele yake tayari kwa kufungwa pingu kwenda kutumikia hukumu yake.

*****MIAKA KUMI NA MBILI ILIYOPITA*****
“Tayari mzigo nimeshautuma, na wale jamaa nimeshamalizana nao.” Ilisikia sauti ya bwana mmoja akiongea na mwenzake kupitia mawasiliano ya simu.
“Sawa, hakikisha pia PZN nilizokuagiza zinawafikia.” Sauti ilisikika upande wa pili.
“Sawa mkuu.” Alijibu hivyo na kasha simu ikakatwa.
“Malkia umeshaongea nae kuhusu kuhamisha wazo? Aliuliza bwana huyo baada ya kumaliza kuongea na simu.
“Hapana sijaongea nae, ila baada ya hapa naenda kuzungumza nae, na lazima kazi hiyo ataikamilisha ndani ya muda mfupi sana.”
“Tatizo lako Jay mambo unayapeleka taratibu sana, hujui kuwa uzembe wako unaweza kusababisha hasara kubwa sana kwetu?
“Sio hivyo, nilienda kwake sikumkuta, na baada ya kumpigia simu akasema aliagizwa Arusha na Mheshimiwa kwenda kumalizana na Yule mkurugenzi mzinguaji. Leo asubuhi anarudi.”
“sasa inakuwaje hakuniaga?”
“Ndio akija umuulize sasa.”
“Hii kazi anatakiwa kuimaliza mapema kabisa vinginevyo tutaumbuka. Wewe hakikisha maandalizi yote yana kamilika kwa upande wako na hayo mengine mwachie mwenyewe.” Alitoa maelekezo hayo bwana huyo aliyeonekana ndiye kiongozi wa vijana hao katika shughuli zao.
“Hilo usijari, kila kitu nimeshakiandaa.” Alijibu Jay kisha wakaagana na kila mmoja akaendelea na shugulia zake.

*****SIKU MBILI BAADAE*****
“BREAKING NEWS: Alfajiri ya leo, Meli ya MV MWANZA imepata ajari na kuzama huku idadi ya vifo mpaka sasa ikiwa ni watu 216 na walio majeruhi ni 7 huku wengine 374 wakiwa hawajapatikana na Jeshi la uokoaji linaendelea na zoezi la kutafuta waliobakia. Ajari hiyo imetokea kilomita 113 kutoka nchi kavu ambapo chanzo kikitajwa ni mlipuko wa mafuta yaliyokuwa ndani ya meli hiyo. Endelea kufuatilia matangazo yetu hapahapa TBC1 ili kujua kila kinachoendelea kuhusu ajali hiyo.”
“Duh! Wewe ni hatari kweli, na mkuu hakukosea kukuita malkia. Yaani kilomita 113 umezimaliza kwa kuogelea.” Alizungumza Jay akiwa anamtazama huyo aliyekuwa anaitwa malkia.
“Unafikiri mimi ni k**a wewe kazi kunenguka na wasichana?” Alijibu Malkia.
“Acha dharau wewe, mbona ni mishe nyingi tu mimi nimezifanya na zote zikafanikiwa. Kufanikiwa kwako hiyo ndio unajiona bora sana.” Alijibu Jay.
“kwani aliyeanza kunisifia ni nani k**a sio wewe pimbi?” Alijibu malkia.
“inatosha. Kwanza hongera Malkia kwa kazi nzuri. Nadhani sasa hivi watu hawatoweza kuongelea kuhusu pesa alizochukuwa mkuu kutoka benki kuu. Watakalia kuzungumzia ajali ya meli huku sisi tukila bata.” Alizungumza kiongozi wao.
“Mishe gani inafuata?” aliuliza Jay.
“Tusubiri tuone hali inavyokwenda sasa hivi kwanza mpaka pale mtakapo pokea maelekezo mengine.” Alijibu kiongozi wao.
*****ITAENDELEA****
JEe! unajua nini kitaendelea katika riwaya hii ya wakili wa kujitegemea? na ilikuwaje mpaka Bw. Nandrie Kweka akamuua mkewe Bi. Mery Sayuni? Usikose sehemu ya pili ya riwaya hii. like kisha share uwezavyo ili na wengine waweze kujua yanayoendelea kwenye page yetu hii.

22/06/2020

Habari yenu wadau wa Story Za Octa. Kwanza kabisa niwatake radhi 🙏🙏🙏 kwa kuchelewesha simulizi. Tangia itangazwe kufunguliwa kwa shule tarehe 29/06/2020. Nimekuwa nikishughulika na maandalizi ya kufungua shule. Ukiachana na uandishi huu. Mimi ni mwalimu na kiongozi, kwahiyo wakati huu mambo yamekuwa mengi hasa ukizingatia hali ya tahadhari ya ugonjwa wa Corona tunayotakiwa kuendelea kuchukua mashuleni baada ya kufungua shule. Niwahakikishie tu kuwa, jumatano ya wiki hii ninakamilisha kila kitu, hapo tutaendelea rasmi na story zetu.

NARUDIA TENA KUWAOMBA RADHI 🙏🙏🙏 WADAU KWA KUSUBIRI PASIPO KUPATA MWENDELEZO.

Pia naomba kuwajulisha kuwa baada ya kufungua shule tutakuwa na madadiriko ya ratiba ya story zetu ambapo, kwa siku tutaendelea kuwa na Riwaya mbili, lakini moja itakuwa inawajia saa tisa kamili mchana, na ya pili itakuwa inawajia saa moja kamili usiku.

KUPOSTI STORI KWANGU NI BURUDANI, SITAKUWA NAMTOZA MTU YEYOTE ILI KUPOSTI STORY LABDA KWA ANAYEHITAJI SEHEMU ZA MBELE. K**A HUNA PESA, HILO USIJARI, WEWE ENDELEA KUFUATILIA HAPAHAPA KWAKUWA TUTAKUWA TUNAPOSTI STORY MPAKA MWISHO WAKE. ILA SUPPORT YAKO YA KUSHARE NA KUWAALIKA WENGINE NI MUHIMU SANA KWAKUWA HAYO NDIYO MALIPO NINAYOYAHOTAJI KUTOKA KWAKO.

NAWATAKIA USIKU MWEMA NA MUNGU AWATUNZE.
🙏🙏🙏

RIWAYA: PANDORA.MWANDISHI: Octa PK.UMRI: 18+Mawasiliano: +255624102400.                         +255746318516.WhatsApp:+...
20/06/2020

RIWAYA: PANDORA.
MWANDISHI: Octa PK.
UMRI: 18+
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
WhatsApp:+255746318516

Wadau wa PANDORA, leo naomba mtufafanulie ili na mimi mtunzi nielewe. Kwenye Simulizi ya Pandora Kuna maeneo k**a, Zukatala, ziwa Vikitii, Bahari ya Hinji, ziwa Yasa, ufalme wa Gulu, ufalme wa Pandora, ziwa Nataloni...Hivi hayo maeneo unaweza kuyafananisha na wapi katika dunia hii? KARIBUNI MNIAMBIE NA K**A KUNA MENGINE ULIYOYAONA NDANI YA PANDORA UNAWEZA KUAMBIA NA KUTUPATIA UFAFANUZI.

KARIBU NA MSHINDI ATATANGAZWA HAPA LEO.

RIWAYA: PANDORA.MWANDISHI: Octa PK.UMRI: 18+Mawasiliano: +255624102400.                         +255746318516.WhatsApp:+...
19/06/2020

RIWAYA: PANDORA.
MWANDISHI: Octa PK.
UMRI: 18+
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
WhatsApp:+255746318516.

*****SEHEMU YA KUMI NA NNE*****

ILIPOISHIA...

"Asante, yaani umekuwa binti mkubwa sasa hivi." Alizungumza Ramia huku akitabasamu na wakati yeye akiendelea kuzungumza Sia alienda kwa Jaran na kumshika mkono kisha wakatoka nje huku wakiwaacha wengine waliendelea mazungumo yao.

"Yaani Sia, nazungumza nae hata hajali, akili yake yote ipo kwa Jaran." Alilalama Ramia.

"Wewe acha tu, kila kukicha analazimisha tuje Kisan nia yake ikiwa kumuona Jaran. Hapo atakuwa amefurahi kweli." Alizungumza Niaya na kuwafanya wote waliokuwa mule wacheke.

"Ehe, naomba mniambie kulikoni na mizigo hiyo msiyohitaji ishushwe?" Aliuliza Dahil.

ENDELEA...

"Ndugu yangu, ujio wetu mahali hapa ni kuja kusema kwaheri, kwani muda wetu wa kurudi Pandora, sasa umewadia." Aliongea Lutas.

"Mbona mapema sana mmeamua kurudi huko, hamuoni kwamba inaweza kuwa hatari kwenu?" Aliuliza Dahil kwa mshangao.

"Hilo lisikupe shaka shemeji. Hatuendi moja kwa moja kwenye jumba la ufalme. Tutaenda kuishi Kijiji cha mbali na jumba la ufalme." Alizungumza Ramia.

"Sasa k**a ni hivyo, kwanini msiendelee kuishi huku, ikiwa hakuna mnachokwenda kufanya huko? Au kuna jambo hamkupendezwa nalo jamani?" Alilalama Niaya.

"Hapana mdogo wangu, tumeamua kufanya hivyo ili Jaran akaendelee kujifunza na kuzizoea mila na desturi za Pandora. Sasa hivi Jaran ana umri wa miaka kumi na moja, na pia mnafahamu yeye ni mzaliwa wa kifalme, hivyo kwa umri wake huo ni vyema akaenda kuishi huko." Alijibu Ramia.

"Sawa, lakini inawabidi mkae hapa usiku huu, harafu kesho muendelee na safari, hakuna haja ya kuwa na haraka kiasi hicho." Alizungumza Dahil na wao hawakuwa budi kukubakiana nao.

Kesho yake kulipo pambazuka walianza safari ya kuelekea Pandora huku wakiiacha familia ya Dahil ikiwa na majonzi kwani walizoeana kuishi na kutembeleana kila mara ndani ya ardhi ya Gulu. Sia yeye ndio wakati wote machozi yalikuwa yanamtoka maana alijua hivi sasa itakuwa ngumu sana kwake yeye kuonana na Jaran k**a ilivyokuwa hapo awali. Waliondoka mahali hapo huku wakiahidiana kutembeleana kila wakati panapo majaaliwa.

Safari ilikuwa ndefu kiasi, na hawakuhitaji kujificha wapitapo mipakani kwakuwa walikuwa na vitambulisho vya Gulu ambavyo vilikuwa ni majina yaliyokuwa juu ya vibao vilivyochongwa kwa usatadi wa hali ya juu huku vikiwatambulisha kuwa ni wafanyabiashara kutoka Gulu. Na kwakuwa ni miaka mingi imepita, haikuwa rahisi kwa wanajeshi wa Pandora waliokuwa mipakani kuweza kuwatambua na hata hivyo wanajeshi wachache sana waliokuwa wakiwakagua, na hao pia hawakuwa makini na maeneo ya mipaka hiyo kwakuwa walikuwa wanakagua watu wanaoingia huku wakiwa katika hali ya ulevi wa kiasi.

Hali ya mahali hapo pa mpakani haikuwa nzuri kabisa hasa upande wa ulinzi k**a ilivyokuwa miaka mingi iliyopita. Wengine walikaguliwa lakini wengine hawakukaguliwa kwakuwa walitoa kiasi kidogo cha sarafu na kuruhusiwa kupita pasipo kukaguliwa.

"Inabidi tuelekee Kijiji cha Kismani, huko hakuna atakayeweza kutugundua na pia ni mbali kabisa na makao makuu ya ufalme wa Pandora." Alizungumza Latus.

"Hapana, kwa hali ninayoiona ndani ya taifa hili. Ulinzi umedorola sana na sio rahisi wao kufahamu uwepo wetu, hivyo nashauri twende tukaishi humo humo Doma, ila iwe pembeni ya mji huo. Na nafikiri itakuwa vyema k**a tutaenda kuishi kijiji cha Zabi." Alizungumza Zulam Maluñ.

"Nahisi wewe pombe bado zinakuendesha kichwani." Yaani unataka tukaishi ndani ya mji mkuu, huoni hiyo ni hatari kwetu? Twendeni huko Kismani ndio pazuri na ni salama kwetu." Alizungumza Ramia.

"Mimi nadhani, alichokiongea Mzee Zulam ni sahihi kabisa, na hiyo itakuwa ni rahisi kwetu kuzifahamu nyendo za maadui kwa sasa. Pia kijiji cha Zabi kipo pembeni kidogo ya mji mkuu wa Doma." Alizungumza Lutas.

"K**a ninyi mnaenda mji mkuu basi tunaachana hapa, mimi na mwanangu tunaenda Kismani, ninyi nendeni huko Doma. Jaran Twende mwanangu." Alizungumza Ramia huku akianza kumuhimiza farasi wake kuondoka, lakini alishangaa Jaran hata hajisumbui kumfuata.

"Wewe Jaran, hujanisikia? Hebu twende."

"Ukiona hivyo ujue, Jaran hahitaji kwenda huko. Twendeni tumuache yeye aende Kismani." Alizungumza Zulam Maluñ ama Zuma k**a alivyokuwa akijulikana Gulu, huku Jaran na Lutas pia wakaanza kumfuata Mzee Zulam wakimwacha Ramia aliyekuwa amesimama peke yake akitazama njia ya kuelekea Kismani.

Ramia hakuwa budi kumgeuza farasi wake na kuanza kuwafuata wenzake huku akiwa hataki hata kusemezana na wenzake kwakuwa hawakumsikiliza. Njiani Lutas, Jaran na Mzee Zulam walikuwa wakifanya mazungumzo lakini Ramia alikuwa kimya.

"Naona roho ya hasira na uchungu wa kulipiza kisasi uliyoiacha miaka ile ulipoondoka Pandora imekutambua baada ya kukanyaga ardhi ya Pandora. Mimi nilifikiri kwakuwa ni miaka mingi imepita basi itakuwa imekusahau, Kumbe bado inakukumbuka?" Lutas aliuliza kwa kumtania Ramia hali iliyopelekea Ramia amtazame kwa jicho la hasira huku akiwa ameuvuta mdomo kwa mbele.

"Mwache, itakuwa tumefanya makosa kuingia hivi ndani ya Pandora, ilibidi tuchinje kuku kuitoa roho hiyo kabla hatujaingia Pandora." Alitania Zulam na kuwafanya wote wacheke isipokuwa Ramia.

"Naona mnataka kuniudhi." Alizungumza Ramia.

"Sio sisi tunaokuudhi, ila itakuwa ni hiyo roho aliyosema Lutas." Zulam alikazia utani wake.

"Mzee Zuma, hivi unajua nimekustahi muda mrefu? Naona hizo pombe zako bado zinakuzuzua akiri. Niache!" Alizungumza kwa hasira Ramia.

"Usiniite Zuma nimeshakuambia, sasa hivi niite Zulam Maluñ, hilo ndilo jina langu. Zuma nimeshaliacha kwakuwa pombe nimeshaacha pia."

"Hahaha, yaani wewe uache pombe? Hilo gudulia la pombe linalokupa mahaba kila siku mpaka unaweseka kila unapotembea, leo useme umeliacha?" Alizungumza Ramia.

"Ndio, nimeliacha Sasa. Tena nataka nikifika Pandora naoa kabisa binti mbichi hivi, ili anizalie watoto." Alimzungumza Zulam na kuwafanya wote wacheke.

"Khaa, kwa uzee huo ni nani ataweza kukubali kuishi na wewe? Huyo atakuwa hajielewi kabisa, na amekosa mwanaume wa kumuoa." Ramia alimtupia neno hilo Zulam.

"Aliyekuambia Mimi ni Mzee nani. Unafikiri sura yangu kuwa hivi ndio kusema mimi ni Mzee?"

"Kwani Mzee Zuma una miaka mingapi?" Aliuliza Jaran aliyeonekana kuwa mkimya muda mrefu.

"Mimi nina miaka kumi na mbili tu." Alizungumza Mzee Zulam na kuwafanya wote waangue kicheko.

"Halafu na wewe, nimesema usiniite Zuma." Alikazia zaidi Zulam baada ya Jaran kumuita jina asilolihitaji kwa wakati huo huku wenzake wakiendelea kucheka.

"Wewe, tena mimi nitaendelea kukuita Zuma na ninashangaa wewe kujiita Zulam Maluñ wakati mimi nilikuwa najua maana tofauti na hiyo." Alizungumza Ramia.

"Ulifikiri maana ya Zuma ni nini?" Aliuliza Mzee Zulam.

"Nilijua maana ya Zuma ni Zulia la Mavi." Alizungumza Ramia hali iliyopelekea Mzee Zuma aongeze mwendo wa farasi wake kwa kasi pasipo kujibu kitu huku na wengine wakianza kufuata kwa kasi huku wakicheka kwa maana aliyoitoa Ramia. Kasi hiyo iliwafanya waufikie mji mkuu wa Doma majira ya jioni ya siku hiyo.
Baada ya kufika Doma ambao ndio mji mkuu wa taifa la Pandora, walielekea moja kwa moja kwenye Kijiji cha Zabi kilichopo pembezoni mwa mji mkuu wa Doma. Walitafuta nyumba ya wageni wakaweza kuipata.

"Ikiwezekana kesho inabidi tutafute nyumba ya kuishi, na pia tunatakiwa kupata vitambulisho vya uraia wa Pandora kwa majina tofauti na tunayoyatumia, vinginevyo hatutaweza kuishi kwa amani ndani ya mji huu." Alizungumza Lutas baada ya kushusha vitu vyao.

"Hilo nitalishughulikia mimi japo mimi siwezi kubadili jina kwakuwa sina ubaya na mtu huku, lakini pia ili kupata nyumba ya kuishi ni vyema tukazungumza na wahudumu wa hapa." Alizungumza Mzee Zulam.

"Sawa, Jaran hebu muite mhudumu wa hapa." Alizungumza Lutas na kumfanya Jaran akamuite mhudumu wa eneo hilo.

"Samahani, kuna nyumba za kununua ndani ya Kijiji hiki?" Aliuliza Lutas.

"Kabisa, tena mna bahati sana. Mjomba wangu anadaiwa na serikali kodi baada ya kushindwa kuilipia biashara yake ushuru ambao serikali ilikuwa imemwambia kulipa, hivyo kuna nyumba yake iko pembeni kidogo mwa Kijiji hiki." Alizungumza mhudumu wa nyumba ile ya wageni.

"Unaweza kutupeleleka sasa hivi.? Aliuliza Lutas.

"Sasa hivi hapana, maana bado nipo kazini. Nitaagiza mtu akamwambie aje hapa, na ninajua atafika mahali hapa maana ana uhitaji mkubwa sana wa pesa."

"Basi, tunaomba utusaidie kwa hilo."

"Sawa." Alijibu mhudumu kisha akaondoka na alilosema alilitimiza kwani majira ya usiku, mjomba wake na yule mhudumu alifika kwenye nyumba hiyo ya wageni, ambapo mhudumu alimpeleka walipokuwa watu wanaohitaji nyumba.

"Huyu ndio mjomba wangu anayeuza nyumba, nadhani mnaweza kuzungumza nae." Aliongea mhudumu yule kisha akaondoka.

"Karibu sana. Sisi ndio tuliokuwa tunahitaji nyumba ya kuishi na bahati nzuri huyo mhudumu ametuambia kuwa wewe unayo na unatafuta mtu wa kuununua." Alieleza Lutas.

"Ninyi mmetokea wapi?"

"Tumetokea Kismani." Alidanganya Lutas ili kuondoa maswali mengi kwa yule mtu.

"Sawa, nyumba ipo lakini inahitaji maboresho kidogo lakini nadhani mtaipenda. Mimi naitwa Jecca, ningependa kuwafahamu majina yenu pia." Alizungumza Mzee Jecca ambapo Lutas alianza kufanya utambulisho kwa majina ya uongo isipokuwa jina la mazee Zulam Maluñ ambaye yeye hakukuwa na tatizo hata k**a atajulikana.

"Sawa, nashukuru kuwafahamu. Kesho nitakuja kuwachukua ili nikawaonyeshe nyumba hiyo."

"Tunashukuru sana, kesho utatukuta mahali hapa." Alijibu Lutas.

"Samahan pia, Jana wakati tunakuja bahati mbaya tulikutana na vibaka wakatupokonya baadhi ya mizigo yetu, ambapo ndani yake kulikuwa na vitambulisho. Tutawezaje kupata vitambulisho vingine?" Aliuliza Mzee Zulam.

"Vitambulisho vinapatikana k**a ukihitaji. Ni pesa yako tu, maana ndivyo tunavyoishi sasa hivi, ukiwa na pesa basi hakuna unachoshindwa kukipata ndani ya mji huu."

"Tutavipata kwa muda gani k**a tukihitaji sasa hivi.? Aliuliza Ramia.

"Mkihitaji sasa hivi, kesho asubuhi mnavipata. Na k**a mna kiasi cha sarafu hamsini au kipande kimoja cha dhahabu, mnapata vitambulisho kwa idadi yenu." Alijibu Jecca.

"Unaweza kutusaidia kuvipata vitamvukisho hivyo?"

"Inawezekana, lakini kila kimoja inawabidi muongeze sarafu tatu. Jumla ziwe sarafu kumi na mbili ikiwa ni sehemu ya malipo yangu."

"Sawa, tunaomba ufanye sarafu kumi kwa vitambulisho vyote." Alizungumza Lutas.

"Sawa." Alijibu Jecca na kumfanya Lutas ampatie sarafu sitini ikiwa ni gharama za kutengeneza vitambulisho na malipo yake.

"Asante, nitakuja navyo kesho." Alizungumza Jecca kisha akanyanyuka na kuondoka eneo hilo.

Kila mmoja alielekea kwenye chumba chake kwaajili ya kupumzika, na kulipo pambazuka Jecca alifika mahali hapo akiwa na vitambulisho vinne vikiwa na majina tofauti na majina yao halisi huku Mzee Zulam Maluñ akiendelea kutumia jina lake halisi.

Baada ya makabidhiano hayo walienda kwenye hiyo nyumba wanayoihitaji kuinunua huku wakiwa wameongozana na Jecca. Nyumba ilikuwa nje kidogo ya Kijiji cha Zabi lakini yalikuwa ni maeneo ambayo kuna makazi mengine ya watu japo hayakuwa karibu karibu Sana. Waliipenda nyumba, na kuamua kufanya makabidhiano ya kimaandishi na muuzaji huku majirani na uongozi wa kijiji wakiwa mashahidi wa makabidhiano hao.

"Tunashukuru sana Jecca." Alizungumza Lutas.

"Nashukuru pia, na k**a kutakuwa jambo lingine lolote msisite kunijuza. Nitawasaidia."

"Sawa." Alijibu Lutas kisha wakaagana. Maisha mapya ya wale wanne yalianza ndani ya Kijiji cha Zabi uliopo Doma ambao ndio mji mkuu wa Pandora.

*****MWAKA MMOJA BAADAE*****

Ni majira ya usiku wa manane, mazoezi makali sana yalikuwa yakiendelea ndani ya msitu wa Imnwe uliopo nje kidogo ya kijiji cha Zabi. Alikuwa ni Jaran na Máulus mmoja wakiambaa angani juu ya msitu ule huku wakiendelea kupigana. Wote walionekana kwenda sambamba lakini mwalimu atabaki kuwa mwalimu tu, kwani Jaran alizidiwa na kupigwa pigo lililomtoa angani na kumpeleka chini, lakini hakuweza kudondoka vibaya kwakuwa alijizungusha kiustadi na kwenda kutua pasipo kuumia.

"Kidogo, umeanza kuwa imara sasa." Alizungumza Máulus yule.

"Aisee, haya mazoezi magumu sana." Alijibu Jaran.

"Usijari, utayamudu vizuri Sana na itafikia wakati ambao hata mimi sitaweza kupigana na wewe tena." Alijibu Mzee Zulam.

ITAENDELEA...

Haya Sasa, Jaran ndani ya Pandora na tayari mazoezi yameshaanza. Unafikiri atakuwaje baada ya mazoezi hayo? Endelea kufuatilia simulizi hii hadi mwisho.

***

SUPPORT NI NDOGO SANA WADAU, WATU WENGI HAWAJISHUGHULISHI NA KUSHARE SIMULIZI. ILA WAPO WACHACHE TU WANAOJISHUGUKISHA NA KUSHARE.
NITAKUWA NATOA POST PALE MUDA NINAOHISI MIMI NDIO UNAFAA KUPOSTI. MTU ASINIFUATE INBOX KUNIULIZA KUHUSU STORY WADAU.

NAWASHUKURU WANAOSHARE LAKINI MUDA SIO MREFU NITAANZISHA GROUO LA BURE HAPA HAPA FB KWA WALE WANAOSHARE NA KULIKE TU, MIMI NAWAONA WOTE WANAOSHARE NA KULIKE NINAWAONA WOTE HUKU.
KWAHIYO WIKI IJAYO WANAOSHARE ILI KUSUPPOT KAZI NDIO NITAKAOWAUNGA KWENYE GROUP LA BURE, NA NINYI MNAOINGIA NA KUSOMA TU MTABAKI HAPA NA STORY ZITATUMWA KWA MUDA NITAKAOUHITAJI MIMI. LAKINI MTAKAOKUWA KWENYE GROUP LA BURE MTAENDELEA KUPATA STORY ZOTE KWA WAKATI.

SIMLAUMU YEYOTE KWA KUWA SIO LAZIMA KUSHARE, NA WALA STAMDAI YEYOTE PESA KWA KUTOKUSHARE, ILA LAZIMA WAFUATILIAJE NDIO WANUFAIKE ZAIDI YA WANAOINGIA KUSOMA NA KUTOKA NDANI YA PAGE HII PASIPO KUSHARE.

ASANTE.

***

Share kadri uwezavyo ili wengine wajue pia kilichomo ndani ya page yetu. Pia hakikisha unawaalika marafiki zako wajongee kwenye ukurasa wetu.

***
Ukitaka uwe wa kwanza Kupata episode ya mbele ni sh. 200/= tu. Na malipo yote yanafanywa kupitia namba zilizopo hapo juu na utatumiwa Riwaya kwa njia ya Whatsapp au inbox kwa upande wa facebook.

RIWAYA: PANDORA.MWANDISHI: Octa PK.UMRI: 18+Mawasiliano: +255624102400.                         +255746318516.WhatsApp:+...
18/06/2020

RIWAYA: PANDORA.
MWANDISHI: Octa PK.
UMRI: 18+
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
WhatsApp:+255746318516.

*****SEHEMU YA KUMI NA TATU*****

ILIPOISHIA...

Masaa machache baadae yaliwakuta mto Ruiche ndani ya pori la Kijiji cha ágáhné. Walikuwa Lutas, Ramia, Mzee Zuma na Jaran pia aliyeng'ang'ania kuwepo mahali hapo kwa ajili ya kujionea yatakayojili mahali hapo.

Wote wanne walikuwa na mavazi meupe ambapo mzee Zuma aliwataka wote waingie ndani ya maji yale yanayopatikana kwenye maporomoko ya mto huo.

Walifanya hivyo huku Jaran nae akiingia ndani ya maji yale ambayo hayakuwa mengi sana eneo hilo walilokuwa kiasi cha kumfanya Jaran ashindwe kuingia. Baada ya kuingia ndani ya maji hayo, mzee Zuma aliwataka watulie pasipo kuyasumbua maji. Mzee Zuma alipoona Kuna ukimya wa kutosha kutoka kwao zaidi ya kelele za mapolomoko na ndege ambao walikuwa K**a burudani kwenye masikio yao, alinyanyua mikono juu kisha akaanza kunena maneno yasiyoeleweka kwa Lutas, Ramia na Jaran lakini kwake yalieleweka na lugha aliyokuwa anaizungumza wakati huo ilikuwa ni Bantu halisi. Mzee Zuma aliendelea kunena na ghafla upepo mkali ukaanza hali iliyopelekea hofu kwa Ramia lakini alijikaza ili asiharibu utaratibu uliowekwa.

Baada ya upepo ule kukata, ilitokea mwanga mkali sana uliowafanya wazuie nyuso zao, na muda mchache baadae walionekana wazee watatu mbele yao huku wakiwa wamesimama juu ya maji pasipo kuzama. Wazee hao watatu kila mmoja alikuwa fimbo mkononi mwake, lakini aliyekuwa katikati yao fimbo yake ulionekana na maua juu yake na kuifanya fimbo hiyo ipendeze sana kuitazama.

Jaran alipomuangalia mtu aliyesimama katikati yao aliweza kumkumbuka kwani ni Mara kadhaa amekuwa akimuota lakini kila akiamka asubuhi huwa anasahau alichokiota, na kila anapotokea mtu huyo ndotoni hunena maneno yasiyoelewe, ndio maana hata Lutas alipokuwa anawasimulia maneno aliyoambiwa alihisi kuyakumbuaka maneno yale lakini hakujua aliyasikia wapi kwa sababu uwezo wa kukumbuka aliyoyaota usiku ulikuwa unaondolewa na miungu ile.

ENDELEA...

"Karibuni, enyi miungu ya Pandora." Alizungumza Mzee Zuma kwa lugha ya Bantu.

"Asante, ewe binadamu uliyejaaliwa kuyajua mambo ya kale. Tunajua kilichowaleta mahali hapa, hivyo kabla hatujazungumza chochote, tunaomba hazina isogezwe mbele." Alizungumza yule mzee kiongozi wao kwa lugha ya Bantu iliyoeleweka vyema kwa Mzee Zuma.

"Bado hatujafahamu hazina ni ipi enyi miungu ya Pandora." Alizungumza Mzee Zuma.

"Hazina ipo katikati yenu ewe binadamu, unashindwaje kuiona?" Kiongozi wa ile miungu alizungumza na kumfanya Mzee Zuma ageuke kuwatazama wenzake na hapo ndipo alipopigwa na butwaa, maana Mavazi na sura ya Jaran iling'aa k**a ilivyokuwa iking'aa ile miungu. Mzee Zuma kuona vile ilibidi atoe heshima kwa Jaran huku Ramia na Latus wakiwa hawaamini wanachokiona kwa Jaran ambapo hata yeye Jaran alikuwa anastaajabu kwa jinsi alivyobadirika huku akijihisi mwepesi kuliko awali. Mzee Zuma alimwambia Jaran asogee mbele yao, na yeye hakuwa budi kufanya K**a alivyoambiwa. Baada ya Jaran kufika mbele ya wote alioambatana nao, yule kiongozi wa ile miungu alipiga hatua kusogea mahali alipo Jaran huku miungu wengine wakiendelea kusimama mahali walipokuwa.

"Ni wakati wako wa kurudi Pandora, kuna mafunzo ya mapigano ambayo sisi tunahitaji kukufundisha. Hatuwezi kukupatia mafunzo hayo ukiwa uhamishoni, hivyo unatakiwa kurudi na kwenda kuyaishi maisha yako nchini Pandora, huko ndiko tutakakokupatia mafunzo ya kujihami." Alizungumza yule kiongozi wa miungu kwa kiswahili fasaha kabisa mpaka Mzee Zuma akashangaa.

"Sijaelewa bado ni nini natakiwa kufanya baada ya hayo mafunzo?" Aliuliza Jaran.

"Ukishafika Pandora, tutakupa mafunzo na kukujuza ni nini unatakiwa kufanya kwa ajili ya Pandora. Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuondoka ndani ya taifa la Gulu na kurejea Pandora." Alitanabaisha hayo yule kiongozi wa miungu kisha wakapotea machoni pao. Baada ya kupotea ile miungu, Jaran alirudi katika hali yake ya kawaida, huku Ramia akimkimbilia mwanae na kuanza kumkagua mwili wake.

"Jaran uko salama?" Aliuliza Ramia.

"Ndio mama niko salama kabisa."

"Hujaungua popote?" Aliuliza Ramia na kuwafanya wote waanze kucheka.

"Sasa mnacheka nini? Hamkuona huo mwanga ulivyokuwa mkali kiasi cha kushindwa kuwatazama?" Alilalama Ramia.

"Hapana mama, niko salama kabisa, hata maumivu hayakuwwpo zaidi ya kujiona nikiwa mwepesi kuliko nilivyokuwa mwanzo." Alizungumza Jaran na kumtoa hofu mama yake.

"Nadhani sasa hazina mmeshaifahamu. Ni wakati wa kuirudisha Pandora na hatuna muda wa kupoteza zaidi ya kufanya hivyo." Alizungumza Mzee Zuma na kuwafanya wote wamtazame.

"Hatuna muda wa kupoteza? Kwani na wewe unaenda?" Aliuliza Ramia.

"Naenda ndio, kwanza Mimi sio mtu wa Gulu. Taifa langu ni Pandora. Kwani nikirudi nyumbani Kuna tatizo?" Alizungumza Mzee Zuma.

"Ooh, kwahiyo huko Pandora unaenda kuishi wapi?" Aliuliza Jaran huku akijizuia kucheka maana alifurahi kuona mzee Zuma akiongozana nao.

"Utakapokuwepo, na mimi nitakuwa hapo." Alijibu Zuma huku akianza kutoka ndani ya maji.

"Haya ewe binadamu mwenye kuyajua mambo ya kale." Alizungumza Ramia na kuwafanya wote wacheke.

Baada ya kutoka mahali hapo walielekea moja kwa moja yalipo makazi yao na hawakutaka kusubiri, kwani walianza maandalizi ya kurudi Pandora.

"Kwani hatuendi kumuaga baba?" Aliuliza Jaran.

"Ndio, tunapitia huko baada ya kutoka hapa." Alijibu Ramia.

"Nahisi Dahil ataumia sana kuona tunaondoka Gulu." Alizungumza Latus.

"Ni kweli kabisa, na hata sisi itatuchukua muda mrefu kuzoea maana ametusaidia Mambo mengi na amekuwa mtu wetu wa karibu sana kwa kipindi chote ambacho tumekuwa hapa Gulu." Alilngezea Ramia

"Hata hivyo, anafahamu kabisa kwamba ilikuwa ni lazima siku moja tutarudi Pandora. Lakini sema imekuwa mapema tofauti na matarajio maana hata Jaran ndio kwanza ana miaka kumi na moja Sasa." Alizungumza Latus.

"Halafu, mimi nashindwa kuelewa ni kwanini hao miungu wanasema turudi Pandora ikiwa bado umri wake ni mdogo." Alilalama Ramia.

"Usitake kuanza kujadili jambo ambalo tayari limeshafanyiwa maamuzi. Na isitoshe miungu imesema sio kwamba anaenda kuanza kazi ila bado anatakiwa kupata mafunzo ili kujiandaa na kazi atakayopatiwa. Hivyo acha kuwa na mawazo ya kutaka kukwamisha zoezi." Alizungumza Mzee Zuma aliyeingia mahali pale na kukuta mazungumzo hayo yakiendelea.

"Wewe nae unajua nini kuhusu watoto, ikiwa kila siku umeendekeza pombe tu hadi ukashindwa kuzaa?" Ramia alimtupia neno hilo Mzee Zuma.

"Kwani aliyekuambia, mimi sina watoto nani?" Alijibu Zuma huku akiweka vitu vyake alivyokuja navyo mahali hapo.

"Hahahahahah, miaka yote upo hapa kijijini unazunguka tu na mipombe yako, huyo mwanamke wa kukuzalia mtoto umpatie wapi? Labda hilo gudulia lako la pombe ulilolifanya kuwa mkeo kila kukicha kulipakata kwapani." Alijibu Ramia.

"Nimeshaacha pombe Sasa hivi, maana najua Kuna kazi kubwa sana ipo mbele yetu. Na kuanzia sasa niite Zulam Maluñ na sio Zuma tena." Alijibu Zuma ama Zulam Maluñ k**a anavyohitaji kuitwa.

Walimaliza kupanga mizigo yao kisha safari ikaanza huku wakitumia farasi katika safari hiyo. Walifika Kanang' majira ya usiku na kuelekea moja kwa moja yalipo makazi ya Dahil. Walifika mahali pale na kumfanya Dahil ashangae kuwaona mahali pale wakiwa na mizigo yao.

"Kulikoni tena, ni safari ya wapi hiyo?" Aliuliza Dahil baada ya kuona wanakataa mizigo yao isishushwe.

"Twende tukazungumzie ndani ndugu yangu." Alizungumza Latus na kumfanya Dahil aanze kuongoza njia.

"Niaya na Sia wako wapo?" Aliuliza Ramia baada ya kufika ndani.

"Wako ndani wamelala, ngoja niagize mtu akawaite maana wanajua tu Kuna watu wamekuja lakini hawajui k**a ni ninyi." Alizungumza Dahil kisha akaagiza kijakazi akawaite.

Dakika chache baadae, Niaya ambaye ni mke wa Dahil na Sia ambaye ni binti yao ila hakutofautiana sana urefu na Jaran waliweza kufika hapo.

"Jamani Ramia, kumbe ni wewe?" Aliuliza Niaya.

"Ndio mdogo wangu, samahani sana tumekusumbua."

"Hata usijari dada. Nimefurahi kukuona mahali hapa." Alijibu hivyo Niaya.

"Shikamo mama." Alisalimia Sia.

"Marahaba binti yangu, haujambo?"

"Sijambo, karibuni." Alijibu Ramia.

"Asante, yaani umekuwa binti mkubwa sasa hivi." Alizungumza Ramia huku akitabasamu na wakati yeye akiendelea kuzungumza Sia alienda kwa Jaran na kumshika mkono kisha wakatoka nje huku wakiwaacha wengine waliendelea mazungumo yao.

"Yaani Sia, nazungumza nae hata hajali, akili yake yote ipo kwa Jaran." Alilalama Ramia.

"Wewe acha tu, kila kukicha analazimisha tuje Kisan nia yake ikiwa kumuona Jaran. Hapo atakuwa amefurahi kweli." Alizungumza Niaya na kuwafanya wote waliokuwa mule wacheke.

"Ehe, naomba mniambie kulikoni na mizigo hiyo msiyohitaji ishushwe?" Aliuliza Dahil.

ITAENDELEA...

Haya Sasa, Hazina ipo inapelekwa ndani ya Pandora, Je! Nini kitajiri huko ikiwa miungu inakwenda kumpatia Jaran mafunzo ya kimapigano? Endelea kufuatilia Riwaya hii hadi mwisho wake.

***

Share kadri uwezavyo ili wengine wajue pia kilichomo ndani ya page yetu. Pia hakikisha unawaalika marafiki zako wajongee kwenye ukurasa wetu.

***

Ukitaka uwe wa kwanza Kupata episode ya mbele ni sh. 200/= tu. Na malipo yote yanafanywa kupitia namba zilizopo hapo juu na utatumiwa Riwaya kwa njia ya Whatsapp au inbox kwa upande wa facebook.

RIWAYA: WAKILI WA KUJITEGEA.MWANDISHI: Octa PK.UMRI: +18.Mawasiliano: +255624102400.                        +25574631851...
18/06/2020

RIWAYA: WAKILI WA KUJITEGEA.
MWANDISHI: Octa PK.
UMRI: +18.
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
Whatsapp:. +255624102400.

Hii ni Riwaya ya kipelelezi, na Ujasusi itakayokuhuzuniasha, kujifariji, kukufundisha. Ni Octa tena ndani ya WAKILI WA KUJITEGEMEA. Octa Atafanya nini ndani ya WAKILI WA KUJITEGEMEA? Unafikiri ni kwanini inaitwa WAKILI WA KUJITEGEMEA? ENDELEA KUFUATILIA PAGE YETU KUANZIA SASA.

MUDA WOWOTE ITAANZA, HIVYO SHARE UJUMBE HUU KADRI UWEZAVYO NA PIA ALIKA WENGINE WAJIUNGE NA PAGE YETU.

HAPA NI BANDIKA BANDUA MPAKA KIELEWEKE.

NAOMBA MJITAHIDI KUSHARE NA KUALIKA WENGINE VINGINEVYO SITOIRUSHA KWA SASA MPAKA WIKI IJAYO.

WAKILI WA KUJITEGEMEA...COMING SOON.

copyright@2020

RIWAYA: KIPANDE CHA WARAKA.MWANDISHI: Octa PKUMRI: 18+Mawasiliano: +255624102400.                         +255746318516....
17/06/2020

RIWAYA: KIPANDE CHA WARAKA.
MWANDISHI: Octa PK
UMRI: 18+
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
WhatsApp:+255624102400.

*****SEHEMU YA MWISHO*****

IILIPOISHIA...

"Kwahyo nafanyaje sasa baada ya hapa?" Aliuliza Octa.

"Ukishabonyeza hiyo alama ya kijani, itakuhitaji kuingiza nyuzi za uelekeo( Longitude na Latitude), baada ya hapo utaweka muda wa kukutana kisha unabonyeza send. Kila mmoja atapata ishara ya eneo la kukutana ambapo kwenye simu ya uliyemtumia kutaonekana ramani na alama nyekundu inayoonyesha sehemu ya kukutana, na muda huo uliouandika ukifika basi kila mmoja lazima afike pale" Luteni Jenerali alieleza kwa kasi sana maana dakika zilikuwa zinazidi kupungua.

"Ni nyuzi gani ambalo mara nyingi huwa mnatumia mmnapotaka kukutana?"

" Ni 64°55'30'S 39°17'06'E." Alizungumza Luteni Jenerali huku hofu ikizidi kuonekana dhahiri usoni pake.

ENDELEA...

"Huu mfumo huwa unawaita wanajeshi pekee au hata wanachama wengine?" Aliuliza Octa.

"Ni wanajeshi pekee." Alijibu Luteni Jenerali huku akifumba macho maana dakika zilikuwa zinaelekea mwisho. Muda ulipokwisha Octa alitabasamu tu maana muda ulipoisha saa ilifunguka yenyewe kwenye mkono wa Luteni Jenerali na kudondoka chini. Octa alimtolea ile saa iliyokuwa kwenye paja lake Luteni Jenerali na akachukua iliyodondoka kisha akatoka kwenye chumba hicho cha mahojiano.

"Tutaonana baadae mzee wangu." Alizungumza hivyo Octa baada ya kifika sebureni.

"Haya poa, nakutakia kheri huko uendako."

"Nashukuru Mzee wangu." Alizungumza Octa huku akifungua mlango na kutoka nje. Octa alielekea moja kwa moja mpaka Ofisini kwa IGP.

"Habari yako mkuu." Alizungumza Octa baada ya kufika kwa IGP.

"Salama, karibu uketi kijana wangu." Alizungumza IGP na Octa hakuwa budi kukaa ili azungumze lkilichompeleka.

"Ndio, nipe ripoti ya ulipofikia" Alizungumza IGP na kumfanya Octa aanze kumwelezea IGP alipofikia hadi namna ya kuwakusanya wanajeshi wa WM.

"Aisee umefanya kazi kubwa sana kijana wangu, hiyo njia ya kuwaita watoke nje ya kambi ndio zuri maana nilikuwa nafikiria ni namna gani ya kuwafyekelea mbali na K**a ingekuwa ndani ya kambi hizo za jeshi, zoezi hili lingekuwa gumu sana." Alizungumza IGP kwa furaha baada ya kuona Octa amefanikisha kazi ile.

"Nimeshawatumia ujumbe wanajeshi wa WM, nadhani ni muda muafaka sasa wa kumuomba jeshi mheshimiwa Rais ili leo usiku tukaliangamize jeshi hilo. Halafu Mimi nitaelekea Bagamoyo kwa ajili ya kwenda kumk**ata Gabriel Phales lakini pia viongozi wote waliomo kwenye orodha hii wak**atwe akiwemo Mr. Rakesh." Alizungumza kwa kirefu Octa ili kuuweka wazi mpango huu.

"Sawa, twende muda huu tukamuone Rais ili kuweza kufanikisha jambo hili." Baada ya maongezi hayo, Inspekta Jenerali wa Polisi Pius Mzava na Inspekta wa Polisi Octavian Peterson wakatoka ofisini hapo kuelekea kwa Rais.

***

Rais akiwa ofisini kwake akiongea na Raphael aliyeonekana kupata nafuu, ghafla simu yake ya mezani ikaita.

"Mheshimiwa Rais, IGP yuko hapa anahitaji kukuona" Alizungumza Katibu muhutasi was Rais.

"Mruhusu aingie" Alijibu Rais na baada ya muda kidogo IGP akaingia akiwa ameongozana na Octa. IGP na Octa wakatoa heshima zao kwa Rais kisha wakaruhusiwa kukaa.

"Karibu sana IGP"

"Asante mheshimiwa Rais, huyu ni yule Inspekta wa Polisi niliyekueleza kuhusu habari zake."

"Ooh, karibu sana Inspekta lakini pia tunashukuru kwa kuliokoa taifa lisipatwe na adha nyingine ya mlipuko. Nimeipata taarifa yako na namna ulivyoingia jeshi la Polisi, na nadhani unatakiwa uingie kwenye kitengo cha TISS ili uungane na mwenzako hapa." Alizungumza Rais na kumfanya Octa atabasamu na kufurahi kurudi kwenye vitengo anavyovipenda sana.

"Asante mheshimiwa, nitafanya hivyo" Alizungumza Octa na kumfanya Rais atabasamu.

"Mheshimiwa tumekuja, na napenda niendelee kutanguliza samahani kwa kuchukua jukumu ambalo walipewa watu wengine, ila nilifanya hivyo baada ya kuona hali ya usalama wa nchi ikiyumba pasipo hata taarifa ya upelelezi wakati kuna kijana anayeweza kuifanya kazi hiyo na ikakamilika."

"Usijari kuhusu hilo IGP, maana ulifanya unalotakiwa kufanya k**a askari unayetakiwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unapatikana. Na ninajivunia sana kufanya kazi na wewe Pius" Rais alitanabaisha yake ya moyoni huku akiwa na furaha.

"Asante mheshimiwa, naomba nikujuze kwamba kazi hiyo imeshakamilika kwa asilimia tisini na nane, na wahusika wote tumeshawapata. Naomba Octa utoe maelezo pamoja na ushahidi wake" Alizungumza IGP huku akimtazama Octa ambaye alianza kutoa maelezo huku akiwasikilizisha sauti, na hakuishia hapo tu aliwajulisha pia namna ya kuwapata watu hao na mpaka anamaliza kuzungumza, Rais alikuwa amekasirika kuliko kawaida hali iliyopelekea avue koti kwa kuhisi joto wakati ofisi ina hewa ya kutosha.

"Kumbe Kuna watu washenzi kabisa kwenye hii nchi, tena wengine niliwaamini kabisa." Alisema hayo kisha akachukua simu na kumpigia waziri mkuu wa wa Uingereza.

"Habari yako mheshimiwa Waziri" Alizungumza Rais wa Tanzania.

"Salama mheshimiwa Rais, habari za huko?"

"Nzuri kabisa, Kuna kesi ya wahujumu wa Muungano wa nchi yetu na mmoja wao anatoka nchini mwako, hivyo nakuomba sana mheshimiwa waziri mtu huyo aweze kushughuliwa" Rais Alizungumza huku akijizuia hasira yake isitambulike.

"Usijari mheshimiwa Rais, tutumie ushahidi huo nasi tutaufanyia kazi." Alizungumza waziri na baada ya hapo Rais alichukua ushahid wote kisha akamtumia waziri mkuu wa Uingereza.

"Hii operation utaiongoza Octa ukisaidiana na Raphael, hakikisheni wabaya wote mnawak**ata na wakibisha waueni" Alizungumza Rais na baada ya hapo akampigia jenerali wa majeshi aliyefika katika ofisi ya Rais nusu saa baadae ambapo alielezwa yote yanayoendelea katika jeshi na nchi pia.

"Naomba jeshi la WM muda ukifika mniachie mimi na wanajeshi wangu, halafu ninyi mshughulike na viongozi wote pamoja na hao wafanya biashara." Alizungumza hayo Jenerali wa majeshi na wao hawakuwa budi kukubali.

Na baada ta mazungumzo hayo Rais alipiga simu uwanja wa ndege kuzuia wahusika wasitoroke na masaa machache baadae oparesheni ya kusafisha wahujumu wa Muungano ilianza ambapo Octa alielekea Bagamoyo kumfuata Mr. Gabriel Phales na Raphael alielekea kwa Mr. Rakesh Sigh, IGP akashughulika na viongozi wasaliti huku Jenerali akienda mahali ambapo wanajeshi wa WM watakutana kwa mujibu wa maelezo ya Octa.

Majira ya saa mbili usiku, wanajeshi wa WM walianza kufika eneo ambalo waliambiwa kufika na kwa kuwa ni utaratibu wao kufika mapema na kumsubiri kiongozi, ndivyo walivyofanya pasipo kujua wamewekwa mtu kati baada ya kiongozi wao kuwekwa kizuizini na Octa. Majeshi ya jeshi la wananchi yakiongozwa na Jenerali mwenyewe yalizingira eneo hilo lenye majengo yaliyotelekezwa huku yakisubiri amri ya Jenerali wa majeshi ndugu Amos Mwampambe.

Jenerali aliruhusu wanajeshi waanze kushambulia, ambapo bila kusita walianza kurusha risasi kwa wanajeshi wale, hakika waliteketea na baada ya nusu saa eneo lote lilikuwa limetapakaa miili ya wanajeshi wa WM ambao hawakujiandaa kwa tukio hilo la kishtukiza kwao. Walianza kukagua miili yote ya waasi wale huku wanaoonekana bado hawajafa wakimaliziwa. Huo ndio ukawa mwisho wa jeshi dharimu la WM(Wapinga Muungano).

***

IGP alianza kupita kwenye kila familia iliyokuwa na kiongozi msaliti huku waliokuwa mikoani wakik**atwa kwa amri ya IGP na askari polisi wa huko baada ya taarifa za wahujumu hao kutumwa huku waliofariki mali zao zilitaifishwa bila kusahau Waziri wa mambo ya nje na Luteni Jenerali wa Jeshi.

***

Octa akiwa na askari wachache walifika mahali anapopatikana Mr. Gabriel Phales mtu mwenye uchu na chuki isiyomuisha mpaka uzeeni. Waliingia ndani ya jengo hilo la kifahari kabisa lililopo pembeni ya mji na kukuta walinzi ambao waliwazimisha. Waliingia ndani na kumkuta mzee ambaye hawezi hata kutembea huku akiwa amekaa kwenye kiti cha mataili.

"Kimbiaaaa" Octa Alipiga kelele ambapo wanajeshi alioambatana nao walitii sauti hiyo na walipotoka nje ulisikika mlipuko mkubwa ulioanza kuishusha chini nyumba hiyo na huo ndio ukawa mwisho wa Gabriel Phales au T001 aliyeishia kujiua mwenyewe.

Siku hiyo wahujumu wote wa muungano walik**atwa akiwemo Mr. Rakesh au WM001, mzee aliyekuwa anatembea mita tatu kwa dakika kumi kutokana na uzee alionao, ambapo mali zake zote zilitaifishwa na serikali huku ikijulikana mali hizo hazikuwa zake bali yeye alikuwa ni kibaraka tu.

***

Nchini Uingereza, baada ya waziri mkuu kupokea ushahidi, aliukabidhi ushahidi huo kwa mamlaka husika na kwakuwa siku nyingi walikuwa wanamtafuta tajiri huyo, hiyo ndo ikawa tiketi ya kumuhukumu. Na kwa mujibu wa sheria za Uingereza za makosa jinai, Mr. Mark Philip au T002, aliweza kuhukumiwa jera kifungo cha maisha.

****************************************************

WAHUJUMU WOTE WA MUUNGANO WA TANZANIA WALIOK**ATWA WALIWEZA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA PAMOJA NA KITAIFISHWA MALI ZAO ZOTE. HUO NDIO UKAWA MWISHO WA WAPINGA MUUNGANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

****************MWISHO*****************

Tuutunze na kuuheshimu Muungano wetu kwani sio wote wanaopendezwa na amani iliyopo Tanzania.

Mwandishi: octa pk.
Mawasiliano: +255624102400.
+255746318516.
WhatsApp: +255624102400.
Instagram: storyzaocta.
Facebook: Story Za Octa.
Email:[email protected].

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255750807702

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ovie posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Ovie:

Share