simulizi_za_kitaa

simulizi_za_kitaa Content creator
Story developer
Script writer

HATIA SEHEMU YA 2MTUNZI: EDWARD BALELE ILIPOISHIAThomas anatoa karatasi kwenye mfuko wake wa suruali,anachukua kalamu na...
13/12/2025

HATIA

SEHEMU YA 2

MTUNZI: EDWARD BALELE

ILIPOISHIA
Thomas anatoa karatasi kwenye mfuko wake wa suruali,anachukua kalamu na kuandika maneno juu ya karatasi kwa herufi kubwa,"NISAMEHE SANA" kisha anafungua dirisha la chumba hiki kilichopo ghorofa ya sita ya hoteli hii na kujirusha.

ENDELEA....

Bibi harusi Paulina bado yupo bafuni akijitazama na kufurahia jinsi alivyoumbika pengine hii ndio sababu iliyofanya vijana wengi wa kiumbe kuongoza kwa idadi kubwa k**a wafuasi wake mtandaoni.

"Baby,mbona unachelewa,mwenzako nina hamu na wewe nataka nikupe vitu adimu na motomoto"Paulina aliendelea kuongea kwa sauti nyororo yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni na kumleta wazi mbele ya kadamnasi ya watu lakini licha ya kujibebisha kiasi hicho hakupokea jibu lolote kutoka kwa Thomas.

Uso wake ukaanza kubadilika ni k**a sasa ameanzw kukasirika maana ni dakika kadhaa zimepita na mumewe bado hajaiingia bafuni. Paulina alitoka bafuni kwa hasira,"Thomas kwani unafanya nini mpaka saa hizi huja...."maneno yalishindwa kutoka kinywani baada ya kugundua kuwa alikuwa anaongea peke yake muda wote aliokuwa bafuni.

"Ameenda wapi huyu,usiku huu?"alijiuliza na kisha upepo ukampuliza mwili na wake na kufanya agundue kuwe dirisha lao liko wazi. Paulina alisogea kwenda kulifunga na kwa bahati anaona umati wa watu wakiwa wamemzunguka mtu aliyekuwa amelala chini na huku baadhi ya watu wakiwa wananyooshea vidole vyao kuelekea dirisha lake lilipo.

Uchungu unamwingia haraka na kupiga kelele,"Thomassss....."anaeguka na kuchukua shuka na kujisitiri mwili wake na kwa bahati mbaya Ile karatasi yenye ujumbe inaanguka chini na upepo unaipuliza na kupotelea chini ya kitanda.

Paulina anateremka chini na shuka lake watu wanamshangaa lakini hajali,machozi yanamtoka. Muda wote analiitajina la mpenzi wake ,ambaye ni mwanaume aliyempenda sana,Thomas.

Anafika chini na kwa nguvu zake anajipitisha katikati ya umati wa watu uliozunguka mwili wa Thomas. Masikini Paulina hofu na mashaka yake vimegeuka kuwa kweli ,ni kweli kuwa aliyelala hapa chini ni mumewe,Thomas Mbuge.
***************************************

NYUMBANI KWA MR MBUGE

K**a nilivyokuambia tangu mwanzo kwamba huu ni usiku mkubwa na sio rahisi kwa wazee wenye umri k**a wa Mr Mbuge kuwa macho hadi muda huu.

Mr Mbuge na mkewe wamelala kitandani,niamini mimi kuwa inahitaji moyo na uvumilivu wa hali ya juu kulala karibu na mwanamume huyu kwani Mr Mbuge k**a usingemjua ungezania kuwa kuna simba ndani ya nyumba hii kwa sababu ya sauti yake ya kukoroma.

Simu yake inaanza kuita na kuwashtua wote wawili. Mr Mbuge anaichukua na simu yake. "Nani tena huyu anayekupigia usiku huu?"aliuliza mkewe,mama yake na Thomas

"Ni mkweo"anajibu Mr Mbuge

"Nani,Paulina?"aliuliza tena mama Thomas

"Ndio,kwani una mkwe mwingine zaidi yake?"

"Anataka nini usiku huu?"

"Sijui,ngoja tumsikilize"

Mr Mbuge anapokea simu na hapo hapo simu inamdondoka mkononi mwake na mshangao mkubwa unajaa kwenye sura yake,Mama Thomas haelewi anamshangaa tu.

ITAENDELEA

simulizi hii itakuwa inakujia Kila baad ya siku moja baada ya sehemu Moja kutoka. k**a unavutiwa na kisa hiki na unapenda kiendelee kupostiwa humu ndani basi usisite ku-like,share na comment ili kunitia moyo zaidi wa kuendelea kufanya hiki ninachokifanya.

Wadau wa mazombi,nipatieni series kali ya mazombi kuzidi hii
13/12/2025

Wadau wa mazombi,nipatieni series kali ya mazombi kuzidi hii

Wangapi mmeiona hii au mnaifuatilia?Kwangu Mimi ni series nzuri ya kuangalia,stori nzuri na wahusika wa kufikirika lakin...
12/12/2025

Wangapi mmeiona hii au mnaifuatilia?Kwangu Mimi ni series nzuri ya kuangalia,stori nzuri na wahusika wa kufikirika lakini inapendeza. Bado wiki moja na siku kadhaa sehemu ya mwisho ya season ya 5 itoke.Mimi mwenzenu naona kuchelewa.

K**a ushawahi kuiona niambie unamkubali nani au umependa nini ndani ya series hii.....


Unafikiri ni kwa nini mara nyingi usaliti unatokea kwa watu wetu wa karibu tuliowaamini?
11/12/2025

Unafikiri ni kwa nini mara nyingi usaliti unatokea kwa watu wetu wa karibu tuliowaamini?

HATIAMTUNZI: EDWARD BALELE SEHEMU YA 1"Hayawi hayawi naolewa,nitarudi nyumbani kutembea"hizo ndizo sauti za shangwe zili...
11/12/2025

HATIA

MTUNZI: EDWARD BALELE

SEHEMU YA 1

"Hayawi hayawi naolewa,nitarudi nyumbani kutembea"hizo ndizo sauti za shangwe zilizokuwa zikisikika nyuma ya Bwana harusi,Thomas Mbuge na bibi harusi mrembo,Paulina Edward zikitoka katika vinywa vya wanawake,wanaume na hata watoto waliohudhuria katika sherehe hii ya kuwaunganisha binadamu hawa wakawa mwili mmoja.

Namna sauti za matarumbeta zinavyofatisha maneno ya wimbo huu hakika ni nani anayeweza kujizuia kuimba,kucheza au hata kutabasamu tu. Hakika wanaume hawa waliovalia sare za polisi wamebarikiwa sana kupiga nyimbo hizi.

Hii ni harusi inayozungumziwa sana huko mitandaoni,Paulina anayejishughulisha na masuala ya urembo na mtoto wa mwisho katika familia ya bwana Edward kitime,huyu ni katibu mkuu wa chama tawala. Paulina ni mtu maarufu huko mitandaoni akiwa na wafuasi zaidi ya milioni tatu kwenye mitandao yake ya kijamii.

Hii ni harusi ambayo wanaume wengi wanatamani siku moja ingekuwa yao lakini kila wakitazama kilichopo kwenye mifuko yao,kinawakatisha tamaa.

Sherehe imefana na watu wamekula na kusaza. Wazazi wa pande zote mbili wanatazama kwa furaha,hakika ndoto za kila mmoja wao zimetimia sasa.

Thomas Mbuge ni mtoto wa mkuu wa jeshi la polisi nchini kitaalamu wanamuita IGP lakini mama yake mzazi ni mbunge wa viti maalumu kupitia chama tawala ndio maana wanaume wengi huko mitandaoni na wenye wivu wanasema ni kwa sababu Thomas anatokea katika familia ya kitajiri ndio sababu amefanikiwa kumnasa binti huyu mrembo sana katika nchi hii.

Muda ulifika na maharusi wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea kuzifurahia siku zao saba za usiku wa mahaba nyie mnaiita "Honeymoon" katika hoteli Moja kubwa ya hadhi ya nyota tano hapa jijini Dar es salaam.

Muda wote ,bibie Paulina alionekana ni mwenye furaha sana na hakudiriki kulifucha tabasamu lake kuonekana usoni. Hii ilikuwa ni siku ya furaha sana kwake. "Nakupenda sana Thomas" alisema Paulina na Thomas aligeuka na kumbusu juu ya paji lake la uso na kumwambia "Nakupenda pia" jibu lililomfanya Paulina azidi kutabasamu na kufurahi.

Maharusi walifika hotelini na kuingia katika chumba kilichopambwa vizuri na bila ya kupoteza wakati,Paulina alimsukuma Thomas kitandani kisha akamrukia na kuanza kumshambulia kwa mabusu motomoto.

Lakini kwa Thomas ilikuwa ni tofauti hakuonyesha njaa hiyo ya kumega tundra lililokatazwa na mti wa katikati akamwambia Paulina,"Tuna muda wa kutosha embu tuoge kwanza mana hili joto nahisi mwili unaniwasha."

"Jamani"Paulina alilalamika lakini akaamua kumsikiliza mpenzi wake huyu,"Basi twende tukaoge wote"Paulina alideka. Thomas alitabasamu na kumwambia,"Haya sawa tangulia bafuni Mimi nakuja"

Paulina alivua nguo zake zote na kubaki k**a alivyokuja duniani na kwa mwendo wa madaha alielekea bafuni.Thomas alitoa karatasi kwenye mfuko wa suruali yake na kuandika maneno juu yake kwa herufi kubwa,"NISAMEHE SANA". Thomas akafungua dirisha la chumba hiki kilichopo ghorofa ya sita ya hoteli hii na kujirusha.....

ITAENDELEA

k**a umependezwa na kisa simulizi hii na ungependa iendelee kupostiwa humu basi like, comment na share mara nyingi zaidi ili kuwafikia watu wengi zaidi. Ukifanywa hivyo basi utanitia moyo wa kuweza kuendelea na hiki ninachokifanya. Asanteni

THE CONJURING Mimi si mdau sana wa filamu za kutisha lakini nimetokea kuzipenda filamu hizi za 'THE CONJURING " kutokana...
10/12/2025

THE CONJURING

Mimi si mdau sana wa filamu za kutisha lakini nimetokea kuzipenda filamu hizi za 'THE CONJURING " kutokana na namna stori yake ilivyokaa na hata uigizaji pia na vile vile napenda jinsi zinavyokufanya muda wote uwe makini kutokana na storyline yake inavyoendelea.

Hizi ni filamu zinazowahusu Ed na Lorraine Warren,mume na mume ambao kazi yao kubwa ni kusaidia familia mbalimbali zinazosumbuliwa na maswala ya kishetani ama mapepo,kuna wakati haya mapepo yanaamua kuwafatilia familia yao wenyewe.

Zipo filamu nyingi zimetoka kufuatia visa hivi vya conjuring na Ed na Lorraine wakiwa wahusika wakuu ni vizuri ukaangalia zote ili uweze kuelewa story nzima.

Filamu hizi zimetokwa kwa sehemu tano na sehemu ya mwisho imetoka mwaka huu yaani bado ni mpya kabisa

👉The conjuring - mwaka 2013
👉The conjuring 2-mwaka 2016
👉The conjuring:The devil made me do it-2021
👉The conjuring:last rites-2025

Mzigo ndio upo hivo,k**a unapenda filamu za kutisha hapo ndio mahala pake😂

# bongomovie

FATHER MATHIAS EP 8ENDELEA...Mganga alianza kupatwa na hofu kitu kilichamshangaza Mathiasi."vipi upo sawa?"aliuliza Math...
14/06/2025

FATHER MATHIAS EP 8

ENDELEA...
Mganga alianza kupatwa na hofu kitu kilichamshangaza Mathiasi."vipi upo sawa?"aliuliza Mathias,
"Hapana,hapana padri siko sawa tangu tulipoachana pale uwanjani siku ya Jana,usiku sijalala kabisa nimekuwa nikisumbuliwa na mavitu ya ajabu ajabu ambayo kwa uwezo wangu wa kitaalamu sikuweza kuvishinda mpaka pale vilipoamua kuniacha venyewe?"alisema mganga.
"Vitu gani vya ajabu?"Mathias aliuliza tena.
"Sijui ni binadamu au lah.Mwili ni k**a wa binadamu lakini wanatembea k**a wanyama.Usiku mzima wamekuwa wakizunguka nyumba yangu sura hazionekani lakini unaweza kuhisi Ile hasira yao"
Wakati wakiendelea kuongea sista Janeth alikuja pamoja na mwenyeketi wa kijiji mzee Jumbe.
"Father Mathias kutana na mwenyekiti wa kijiji,Mzee Jumbe"alisema sista Janeth.
Father Mathias alinyanyuka na kusalimiana na mwenyekiti

"Habari yako father"alisema mzee Jumbe
"Salama mwenyekiti,heshima yako"alijibu Mathias
"Nimeipokea,bila kupoteza muda ujio wetu hapa ni k**a ambavyo umesikia ,kijiji chetu kimekuwa kikiandamwa na mambo yasiyoelezeka ila Kwa sasa tunataka tuanze na Jambo la msingi ambalo limetuathiri Kwa kiasi kikubwa" alisema Mzee Jumbe
"Sawa,nakusikiliza"alidakia Mathias
"Tumeongea na viongozi wa dini katika kijiji chetu kufanya Ibada ya pamoja katika uwanja wa zahanati yetu ya kijiji ili tuweze kuwasaidia mabinti zetu waliokumbwa na balaa la kupoteza fahamu katika zahanati yetu,hivyo Kwa sababu wewe ni mgeni hapa nikasema ni vyema nikaja mwenyewe ili nikuombe tuongozane"alimalizia Mzee Jumbe

Mathias alikaa kimya kwa sekunde kadhaa akitafakari kisha akafanya maamuzi,"sawa nimekubali tutaongozana mimi na wewe mpaka zahanati ila kwa sasa kuna jambo natakiwa kulifanya"Mathias alisema na kisha kumgeukia mganga,"Je,upo tayari Kwa ubatizo"aliuliza
"Sasa hivi?"Mganga aliuliza
"Ndio,Imani yako ndio itakayokuponya."
"Nipo tayari"alisema mganga.

Father Mathias aliagiza maji yaletwe kisha akayabariki na kisha kumbatiza mganga.
ITAENDELEA

Hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kipindi kile nasoma sema tu sikuwaga na nguvu🤣🤣🤣
13/06/2025

Hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kipindi kile nasoma sema tu sikuwaga na nguvu🤣🤣🤣

FATHER MATHIAS EP 7ENDELEAFather Mathias anashangaa kumuona paroko akiwa hajiwezi kitandani mwake,macho yake yanashindwa...
13/06/2025

FATHER MATHIAS EP 7

ENDELEA
Father Mathias anashangaa kumuona paroko akiwa hajiwezi kitandani mwake,macho yake yanashindwa kuamini hiki anachokiona.Anaamua kumsogelea paroko karibu ili kuona k**a ni kweli hajiwezi au anaigiza lakini kabla hajamfikia anashtushwa na mguso wa mkono kwenye bega lake,"Mungu wangu"anashtuka na kugeuka.

Mbele yake ni sista Janeth amesimama,"vipi Baba mbona upo hapa muda huu?"sista Janeth aliuliza
Father Mathias anapatwa na kigugumizi hajui aseme nini.
"Niliona mtu ananiingia humu ndio maana nikamfata kumbe ni wewe?"aliongeza sista Janeth
"Ni kweli nilikuwa nje nikipunga upepo nikaona sio mbaya kuja kuona anaendeleaje."alisema Father Mathias.
"Sawa"sista Janeth alijibu na kuondoka chumbani humo.Father Mathias naye akarudishia mlango na kutoka.

Mathias baada ya kurudi chumbani kwake alikaa juu ya kitanda na kutafakari bila ya kupata majibu.
***************
Asubuhi ilifika na kila kitu kilionekana kiko sawa.Father Mathias aliamka na kuanza kutembea tembea ndani ya eneo la kanisa.Alifika sehemu ambapo kuna mti mkubwa wa kivuli na kuamua kukaa chini yake.Mbele yake anamuona sista Janeth akiwa ameongozana na mwanaume mmoja,"Tumsifu Yesu kristu"alisalimia sista Janeth."Milele Amina"alijibu father Mathias.
"Baba, una mgeni wako amekuja kukuona"alisema sista Janeth
"Mgeni wangu mimi?"Mathias aliuliza
"Ndio"Janeth alijibu na kumkatibisha yule mwanaume aje karibu na Mathias.

Father Mathias alimtazama vizuri yule mwanaume na kumkumbuka,alikuwa ni yule mganga aliyemsaidia jana yake.
"Ni wewe?"Mathias aliuliza
"Ndio"mganga alijibu
Sista Janeth aliaaga na kuamua kuwaacha peke yao
"Samahani baba padri,nimekuja hapa nataka kubatizwa"alisema mganga
Mathias alistaajabishwa na kauli hii iliyotoka Kwa mganga"kubatizwa ,wewe!"mshangao
"Ndio padri,nataka kubatizwa"aliongeza mganga
"Ni kitu gani kilichopelekea kufanya uamuzi huu?"aliuliza Mathias
Swali hilo likapelekea kurejesha kumbukumbuku za kutisha katika fikra za mganga.Mganga akaanza kuingiwa na hofu.

FATHER MATHIAS EP 6MTUNZI: EDWARD BALELEENDELEA Basi Sista Janeth akishirikiana na yule sista mwingine walibeba mizigo y...
13/02/2025

FATHER MATHIAS EP 6
MTUNZI: EDWARD BALELE

ENDELEA
Basi Sista Janeth akishirikiana na yule sista mwingine walibeba mizigo ya Mathias na kumuonyesha chumba chake ambacho atakuwa anaishi kwa kipindi chote atakachokuwa mtovolwa.
Baada ya kuweka kila kitu sawa Mathias aliamua kwenda kumuona Paroko wa mtovolwa ambaye alisikia kuwa amerejesha fahamu.Alienda hadi kwenye chumba cha Paroko na kubisha hodi.Mlango ulifunguliwa na sista Janeth akatoka,"Father Mathias,Karibu?"alisema sista Janeth.
"Asante,nimeona nije kuona Paroko anaendeleaje?
"Sawa hamna shida,ingia ndani"
Wanaingia ndani na kitandani alikuwa amelala mwanaume mzee Sana.
"K**a unavyoona ,ameweza kufumbua macho ila hawezi sema neno lolote."alisema sista Janeth.

Mathias anachukua msalaba wake na kuuweka katika paji la uso la Paroko na kumuombea.Baada ya kumaliza kuomba alirudisha msalaba wake."Mungu ni mwema atatenda kwa kadiri ya mapenzi yake."
"Amina" aliitikia sista Janeth.
******

Masaa yalikwenda na usiku ukaingia.Mathias akiwa chumbani kwake anasoma biblia.Ulivuma upepo kidogo na umeme ukakatika."Umeme wa nchi hii!"alijisemea Mathias.Akaweka biblia yake vizuri na kupanda kitanda na kulala.Baada ya kupanda kitandani mlango wa chumba chake uligongwa."Nani",aliuza Mathias lakini hakupatiwa majibu.Mathias akaona isiwe tabu ngoja niende kufungua mlango.
Alifungua mlango na hakufanikiwa kuona mtu yoyote."Au naota?"alijisemea na kufunga mlango,wakati anageuka alishtushwa na kumuona Paroko amekaa kitandani kwake.
"Niliambiwa huwezi kutembea umefikaje hapa?"aliuliza Mathias lakini badala ya majibu alipokelewa na kicheko cha kejeli kutoka kwa Paroko kisha parako akasimama"unapaswa uondoke katika kijiji hiki na usipofanya hivyo utakufa"Paroko alimwambia Mathias na kupetea kimiujiza na hapo hapo umeme ukarudi.

Bila kupoteza muda Mathias alitoka na kukimbilia kwenye chumba cha Paroko na kufungua mlango.Hakuweza kuamini alichokiona , alimkuta Paroko akiwa amelala kitanda hajiwezi k**a alivyomuona asubuhi.
***

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255719997985

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when simulizi_za_kitaa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to simulizi_za_kitaa:

Share

Category