B DADI

B DADI kwa movie na musiki tunapatikana you tube kwa maelezo zaidi tufollow instagrame na b dadi kwa music ni mdundo. com na sound cloud ni b dadi audio mack b dadi

28/10/2025
25/10/2021

*JIFUNZE KITU*

Amekutext inbox WhatsApp 📩

Ukamuuliza we nani? 🤷‍♀

Akakujibu jina🤦‍♂

Ukamuuliza umepata wapi namba yangu?🤷‍♀

Akakujibu, nimepata kwenye lile group tupo wote🤳

Ukachukulia poa tu🧕

Ulivyoingia fb ukakuta amekutumia urafiki 'Friend Request' facebook

Ukam Confirm

Ukaingia katika Timeline yake.

Ukaangalia picha zake

Ni mkaka handsome

Anaendesha Range

Anaonekana ni jamaa mwenye uwezo

Akakutumia text messenger

Ukamjibu

Mkachat sana kufahamiana zaidi

Akakuomba umtumie picha zako

Ukamtumia

Akakusifia jinsi ulivyo beautiful

Ukasema, "Kawaida kaka"

Siku kadhaa zikapita

Akakutext tena

Ukafurahia kuona text yake

Mwishowe akafunguka kuwa amekupenda

Hukuamini

Akakakuhakikishia kweli anakupenda

Ukamwamini na kumkubalia

Ukawa unamuomba akutumie pesa za kutumia

Akawa anakutumia zaidi ya ulichoomba, umeomba 5000 sms ya TIGOPESA inakuja 20,000

Ukaona hapa mwanaume nimepata

Ukawa unapost picha zake fb na kwenye status yako WhatsApp picha zake hazikukoma

Akakuomba muonane

Mkapanga kuonana

Ukamwambia atume nauri.

Bila kuchelewa sms ya TIGOPESA ikalindima kwenye simu yako. 200,000 ni nauri umetumiwa ingawa unapotokea na unakokwenda haizidi 70,000.

Ukajikwatua mwenyewe

Ukaenda kusuka kwenye ile saluni yako unasukagwa sikuzote

Ukawaambia wakusuke vizuri kabisa maana unaenda kuonana na kingboy wako

Ukajipulizia na marashi ya kunukia vyema

Ukaweka na make-up na weave mpya.

Ukapanda usafiri.

Njiani hakuacha kukusalimu na kujua umefika wapi

Hatimaye safari yako ukafika.

Akaja stendi kukupokea

Akakuchukua kwa ajili ya lunch kwa hotel

Akakuagizia na soft drinks

Mkawa na muda mzuri pamoja

Akakushika mkono

Akakufanya uwe unacheka muda wote kwa vituko vyake

Ukampenda mno

Ikawa k**a umemjua kwa miaka

Akakuchukua kwenda kwake

Akaweka mazingira ya wewe kujisikia upo kwako kwa kukuruhusu ulale kitandani kwake

Akakubusu kimahaba

Ukapenda jinsi alivyo romantic, nguvu na ujasiri

Ukajisikia secure ukiwa nae

Akaanza kukupapasa matiti yako taratibu

Ukajua kuwa unachoenda kufanya sio sahihi lakini ukajisikia poa tu

Ukamwambia mtumie kinga, akakuambia 'haitaleta utamu baby'.

Ukamkubalia maana hukutaka kumsumbua.

Akakuambia anakupenda na hukusita kumwambia unampenda pia.

Baada ya kumaliza akafungua friji na kukunywesha maji ya kunywa.

Ukajihisi hapa mume nimepata

Ukajihisi ni mwanamke special

Atakuwa ndio yeye uliyekuwa ukimuota siku zote.

Akaanza kukuvua bikin zako taratibu

Nawe ukaanza kumvua bukta yake huku ukimtazama kwa jicho lilolewa mahaba

Mkaangushana kitandani

Mkaanza kufanya

Wakati wa shughuli ulijihisi dunia nzima unaimiliki wewe

Kwani alikuwa akikupa raha ambazo hukuwahi kupewa na mwanaume yeyote

Hatimaye ukafikishwa kilele cha mlima Kilimanjaro ukiwa na tabasamu nono

Ukamwambia "Aksante hubby kwa sexy tamu mno"

"Usijali ma queen" akakujibu huku akikubusu shavuni

Ukavaa nguo

Siku ikapita

Kesho yake ukaomba urudi home

Akakuchukua mpaka sehemu zinakopaki mabasi

Akakubusu tena katika shavu. "Nimekuwa na muda mzuri na wewe" akakueleza.

Akakupa Tsh 300,000

Ukatabasamu na kumwambia tutaendelea kuwasiliana baby

Akabaki kimya.

Ndani ya basi uliyopanda ikaanza kuondoka.

Ndani ya basi hukuacha kutabasamu

Ukafika nyumbani kwenu na kumwandikia text WhatsApp kwamba umefika salama.

Yupo online lakini hakujibu text yako

Ukaamua kumtext tena, hakujibu!

Dakika chache baadae humuoni WhatsApp unaona kivuli tu. AMEKUBLOCK!!

Ukaingia fb nako amekublock

Messenger nako vilevile

Hukujua kwa nini lakini

Uliumia mno

Siku, wiki, miezi ikapita ukaanza kujisikia homa homa, mchovu, uzito umepungua

Ukaenda kituo cha afya

Ukapima

Nusu saa baadae daktari anaingia.

"Pole sana dada yangu" daktari anakuambia.

"Una maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ni mjamzito vile vile".

Mimba, HIV+????

HOW???

Hauelewi

Inakuumiza sana,

Hauamini.

Unaenda nyumbani.

Ukiwa na hofu kubwa.

Unaona kifo hichi hapa

Unatazama angani, na unauona mwisho wako huu hapa. Unajuta kumuamini mwanaume yule kirahisi hivyo.

[ MWISHO ]

Najua vipo visa vingi vya wasichana waliotendwa vibaya na wanaume wa mitandaoni wasio wastaarabu, lakini kisa cha leo kitoshe kukupa somo kamili na kujihadhari.

Cha mwisho, msitangulize sana pesa mbele kuliko mapenzi. Katika post hii haimaanishi wanaume wote wa mitandaoni ni wabaya, la wapo na walio wema, ila kinachokuja kuwafanya mjikwae wasichana wangu, ni ile hali yenu ya kuweka mbele pesa kuliko mapenzi ya kweli. Wapo wanaume wenye uwezo humu mtandaoni ambao wao pesa ipo na hawaoni hasara kukupa wewe chochote unachohitaji ilimradi tu umempa sexy.

Lakini pia wapo wanaume humu ambao wao hawana pesa mnazozitaka LAKINI wana mapenzi ya kweli na wana nia njema wanapowafuata inbox; kinachowatenganisha tu ninyi na wao ni pesa. Maana umemuomba akutumie 10,000 ya soda, anakulilia kuwa dada hali ngumu, sina hiyo 10,000. Akija tena kuangalia inbox anakuta umeshamblock

K**a utakuwa umesoma kwa makini post hii, kilichomwangamiza dada huyu sio yule mwanaume bali ni kule kupenda pesa. Utakuta mwanaume amechat nawe leo tu, kesho umemwomba akutumie 15000 ya kwenda kusuka. You can't be serious ... Utakuja kuumia. Wapo wanaume walio na uwezo kuwapa pesa, lakini kumbukeni hawatawapa bure, msiwe wepesi kutanguliza pesa za wanaume wa mitandaoni, pesa zingine mbaya zitakujaga kuwatokea puani.

Dada zangu, jifunzeni kitu kwenye kisa hiki. Ushauri wa bure
Shea post hii ili wengine wajifunze.

22/09/2021

Msanii wako unae mkubali yupo mtaani anakuwakilisha vyema show love kwa mtaa na pia masnitch tunawakataa Kiana Haina fagio hapa

Sina kesi
07/09/2021

Sina kesi

22/07/2021

STORY:KATOTO KENYEWE KABAYA, NANI ATAKACHANGIA, ANGEKAACHA KAFE TU!*

Tofauti na watu wengine ambao wakimaliza chuo wanahangaika kupata kazi mimi haikua shida kabisa. Nilizunguka mara mbili tatu nikapata kazi katika kampuni moja kubwa tu. Sikutarajia kwani sikuwa na uzoefu kabisa, niliingia kazini na kufanya kazi vizuri tu, bosi wangu alikuwa ni mtu poa sana. Kampuni ilikuwa ikimilikiwa na mtu na mke wake lakini mke ndiyo alikuwa anasimamia kila kitu.

Siku tu ya usaili yule dada alinichangamkia sana, sikuwa na uzoefu lakini nilishangaa napata kazi tena kwa mshahara mzuri. Nilipoanza kazi alikuwa karibu yangu sana, alikuwa ananisaidia kukua, ananishirikisha kwenye mambo mengi na dili zote za pesa alikuwa akinishirikisha. Nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na mambo yangu yalikuwa mazuri nilijiona kabisa napanda cheo.

Siku moja Bosi wangu alinikaribisha kwake, pamoja na mazoea na wafanyakazi wake lakini hakuwa mtu wa kumkaribisha mgeni kwake. Nilikuwa nalielewa hilo na kikubwa nilisikia kuwa pamoja na pesa zao nyingi lakini walikuwa hawajabarikiwa kupata mtoto, walishakuwa naye lakini alifariki akiwa na miaka mitano.

Mtoto wao alizaliwa na matatizo ya moyo na figo, walihangaika naye sana ktk hospitali mbali mbali na nilisikia kuwa kuna kipindi walikaribia hata kufunga kampuni kwani walishauza kila kitu ili kugharamia matibabu lakini mtoto wao alifariki dunia na hawakubahatika tena kupata mtoto. Hiyo ilikuwa ni miaka mitatu nyuma. Nilifurahi kukaribishwa, nilifika aliniandalia vizuri, mume wake hakuwa nyumbani.

Basi nilikaa. Ukutani kulikuwa na picha kubwa ya mtoto wao, niliiangalia naye akaanza kunitambulisha kwa mtoto wake kupitia ile picha. Akaniambia jinsi alivyohangaika naye mpaka kufia mikononi mwake. Aliongea huku akilia, nilimuonea huruma. Kwa kuingalia ile picha tu mtoto alionekana anaumwa sana.

Wakati tumekaa alinionesha albam ya picha za mtoto wake. Alinionesha picha nyingi sana mpaka picha nyingine wakiwa hospitalini, akiwa amempakata mtoto wake ana hali mbaya, picha za mazishi, alikuwa akilia wakati wote mpaka mimi nikalia. Mwisho alinyamaza ghafla, akachukua simu yake, akafungua kitu kisha akaniambia.

“Maombi yako yalitimia, mtoto wangu alikufa k**a ulivyotamani iwe” aliniambia, nilish*tuka kwani sikudhani k**a ningeweza kufanya hivyo.
“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza kwa mshangao. Hakutaka kuongea sana, aliingia Facebook, sijui alifanya nini ni k**a alikuwa kaandaa hiyo post akanionyesha Comment yangu ambapo nilicomment miaka k**a mitatu au minne nyuma kipindi hicho nikiwa chuo mwaka wa kwanza.

Kuna group ilipostiwa picha ya mtoto wake akiwa anaumwa anaomba mchango kwa ajili ya matibabu na mimi nilicomment *“Katoto kenyewe kabaya nani atakachangia angekaacha kafe tu!”* Ilikuwa ni comment ya zamani, yaani hata nilikuwa siikumbuki. Niliishiwa nguvu kwani kwenye hiyo post ni mimi tu niliongea hivyo, watu walinichamba sana lakini niliishia kuwatukana na kuzidi kumtukana mtoto ili tu kujionyesha mbabe.

“Jina lako siwezi kulisahau, nilijuta hata kuomba msaada kwani baada ya wewe kuandika vile pamoja na kupata pesa lakini haikupita wiki mtoto wetu alifariki dunia. Machungu niliyoyapata nilishindwa kukusahau, ndiyo maana nilipokuona umekuja kuomba kwenye usaili pamoja na kwamba hukuwa na vigezo nililazimisha kukuajiri ili kukuonesha kuwa *maisha yana kesho….”*

Aliongea mambo mengi sana kwa uchungu, nilimuomba msamaha kuwa niliandika tu kiutani na sikudhamiria. Yeye hakuwa na neno, aliniambia amenisamehe ila alitaka tu kunifundisha maisha. Nilishindwa hata kukaa, nilinyanyuka na kuondoka. Hakunifukuza kazi lakini sikuweza tena kurudi pale kazini. Niliacha kazi sikurudi hata kudai kitu chochote.

Alijaribu kunitafuta ili nirudi kazini lakini sikuwa na huo ujasiri, nilikua naogopa sana kiasi kwamba nilidhani k**a nikirudi anaweza kunifanyia kitu kibaya. Nina mwaka wa pili sasa tangu niache hiyo kazi na bado sijapata kazi nyingine. Maisha yamekuea magumu sana, mpaka leo najuta, unaweza kuongea kitu k**a utani au kutaka sifa kwa watu bila kujua unaharibu maisha ya wengine au kuwasababishia maumivu makubwa sana.

MWISHO

TUWE MAKINI SANA NA TUYAFANYAYO HAPA DUNIANI.MAISHA YANA KESHO.

*Tunaishi katika dunia ambayo watu wasio na pesa wanatafuta pesa ili wapate furaha, wakati huo watu wenye pesa wala hawa...
02/07/2021

*Tunaishi katika dunia ambayo watu wasio na pesa wanatafuta pesa ili wapate furaha, wakati huo watu wenye pesa wala hawana furaha na pesa zao.*

*Hii ni dunia ambayo maskini anakula chochote anachokipata akisononeka kuwa angekuwa na hela, labda angekula vizuri zaidi. Lakini yupo tajiri anayekula mchicha wa kutandika kwasababu ya maradhi yanayoushambulia mwili wake.*

*Kuna mtu yupo hospitali anazungumza na daktari kwa siri amsaidie kutoa mimba, halafu kuna mwingine yupo chumba cha pili anamuomba daktari amsaidie mwaka wa saba huu hajapata mtoto.*

*Kuna mtu yupo sehemu fulani ya dunia anatia saini hati ya talaka kuwa haitaki tena ndoa yake. Lakini kuna mtu yupo kanisani amepiga magoti anamuomba Mungu ampatie mume.*

*Nimejionea sana kipindi nasoma, kuna wanafunzi wanatamani kusoma lakini wanaondoka shule kwasababu wazazi wamekosa ada, lakini kuna wanafunzi wanaondoka shule kwasababu wazazi wanawataka wakisimamie Biashara zao.*

*Kuna mtu sasa hivi anaandika barua ya kuacha kazi kwasababu kazi yake imemchosha. Halafu kuna mtu anabadilisha bahasha ya kuhifadhi vyeti vyake, mwaka wa sita huu hana ajira.*

*Nimejifunza sana kutoka kwa watu maarufu. Kuna mtu sasa hivi anaumiza kichwa usiku na mchana atakuwaje maarufu afahamike na kila mtu mjini halafu yupo staa anayetamani kushuka kwenye gari aingie japo mtaani kuzurura lakini hana hiyo nafasi tena.*

*Kuna mzazi sasa hivi anatamani muda urudi nyuma ili akamfunze mtoto wake maadili, halafu kuna mzazi analia amempoteza mwanae, baada ya kumlipia ada na kumpatia malezi mazuri kwa miaka yote, leo amekunywa sumu kwasababu ya mpenzi aliyekutana mwaka jana.*

*Nilijionea nilipokuwa shule, kuna mwanafunzi analia kupata C akiamini amefeli sana lakini kuna mwanafunzi anayerisiti miaka wa tatu anaitafuta hiyo C.*

*Hata ninapomaliza kuandika haya, kuna mtu anasoma akiamini hiki ni kitu chema kwake lakini yupo anayeona hili andiko ni ujinga na upuuzi tu.*

*Lakini Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa, kila kitu kina upande wake wa pili wa maisha. Unachoona bora kwako kwa mwingine kinaweza kuwa takataka. Kinachoweza kuwa takataka kwako kwa mwingine kinaweza kuwa bora. Kwahiyo, tuishi maisha yetu tuliyopewa na Mwenyenzi Mungu.....🙏* Naitwa bdady mkali wa mipasuko msanii mkubwa link kwa bio

KIJIJI CHA GAMBOSHI KINACHODAIWA NI KITOVU CHA UCHAWI KANDA YA ZIWA Kijiji cha Gamboshi, ambacho kwa miongo mingi kimeku...
01/07/2021

KIJIJI CHA GAMBOSHI KINACHODAIWA NI KITOVU CHA UCHAWI KANDA YA ZIWA

Kijiji cha Gamboshi, ambacho kwa miongo mingi kimekuwa kikiogopwa k**a makao makuu ya wachawi na uchawi wa kutisha.

Kimekuwa ni kijiji kinachotafutwa na watu
wanaotaka utajiri na uongozi kwa njia ya mkato.

Mwandishi wa habari hii amejikuta akipata wakati mgumu kutoka kwa wasak**ali na uongozi tangu alipoandika habari za kijiji hicho katika vyombo vya habari.

Haileweki ni vipi watu hao waliweza kupata
namba yake ya simu kwani kati ya March 12 hadi May 28, aliweza kupigiwa simu na
watu 19, na 11 kati ya hao wakitaka awapeleke au awatajie majina ya ‘Wazee’ maarufu watakaowawezesha kufanikisha malengo yao wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Huku 8 waliobaki wakiwa ni wachimba madini ambao wanaamini
wazee wa Gamboshi wanaweza kuwaonesha madini yalipo.

“Nasikia wewe ndiye unawapeleka watu
Gamboshi, tafadhali nisaidie nikawaone ili
waninyoshee mambo yangu. Mimi niko Mererani Arusha,” alisema mmoja wa watu hao katika simu aliyompigia Mwandishi wa habari hii.

Mwingine aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Dodoma alisema: ” Bwana naomba nisaidie nifike Gamboshi ili wataalam hao wanisaidie katika uchaguzi ujao, kuna jimbo la uchaguzi nalowania".

Kwa mujibu wa wakazi wa kanda ya ziwa, Gamboshi si mahali pa kupakimbilia kwani kijiji hiki kimetajwa kuwa na mengi ya kutisha kiasi cha kuitwa ni ‘jiji
la miujiza’.

Moja ya visa vilivyowahi kuripotiwa na ambavyo viliwaogopesha sana watu ni pamoja na viongozi wa kiserikali na kichama kunyolewa nywele
sehemu za siri, kujikuta wamelazwa nje.

“Gamboshi si mahala pa kutembea kwa sababu ukienda kamwe hutarudi, nawafahamu vema wakazi wa huko si rafiki kabisa na watu wengine,” alinionya Epaphra Swai, mkaguzi wa
viwanda vya kuchambua pamba mkoani Simiyu.

Kijiji hicho ambacho ni nadra sana kutembelewa, kimepata umaaurufu mkubwa ndani na nje ya
nchi k**a k**a kitovu cha uchawi na
wachawi wanaoweza kufanya miujuza, hali
ambayo imekifanya kijiji hicho kupitwa na
mkondo wa kimaendeleo kitaifa.

Hata hivyo baada ya kukitembelea kijiji hicho, wakazi wake walidai kuwa mengi
mabaya yanayosemwa dhidi yao ni ya kuzusha tu, na chumvi nyingi kuongezwa, hali ambayo imeathiri maendeleo ya kijiji chao.

“Sisi ni wakulima wakarimu wa pamba, mahindi na mpunga. Yote mnayoyasikia kwamba sisi ni magwiji wa uchawi ni uvumi uliotiwa chumvi nyingi. Tunamuomba Rais wetu kwa kushirikiana
na mbunge wetu, Andrew Chenge atusadie
kulisafisha jina letu,” alisihi Zephania Maduhu, afisamtendaji wa kijiji cha Gamboshi.

Maduhu pamoja na wanakijiji wenzake walidai kuwa hofu iliyoenezwa kitaifa na kimataifa juu ya uchawi uliovuka mipaka wa kijiji cha Gamboshi umesababisha madhara makubwa kwa kijiji hicho
kiasi cha kutengwa na jamii yote ya Watanzania.

“Hakuna aliyetembelea kijiji hiki kwa miaka mingi sana. Hata sisi tunapotoka nje ya kijiji wengi hawataki kutusogelea wakiamini
tuwadhuru, ” alisema Musa Deus, 26, mmoja wa wakulima walionufaika sana kilimo cha mkataba kijijini Gamboshi.

Kwa mujibu wa afisa mtendaji,
tangu Uhuru hakuna kiongozi yoyote wa kitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo. Mtu wa pekee aliyewahi kuzuru kijijini hapo ni mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, ambaye alifika kijijini hapo mwaka 2010 wakati akifanya kampeni
za ubunge.

“Tume ya katiba ilitupita, mwenge wa Uhuru nao haujawahi kupita hapa. Tuko kisiwani mbali na Watanzania wengine,” aliseman afisa mtendaji.

Mijini na vijijini, kumekwepo na ubishani mkali kuhusu ni mkoa gani unaokimiliki kijiji hicho ambacho baadhi ya wakazi wake wanadai kuwa miongoni mwa vioja vyake ni mauzauza yanayoweza kuifanya Gamboshi ionekane k**a jiji la New York au London wakati wa usiku.

Wakazi wa Shinyanga wanadai kuwa Gamboshi iko wilayani Magu, mkoa wa Mwanza, wakati wale Mwanza wakidai kuwa iko mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa afisa mtendaji, Gamboshi iko katika wilaya Bariadi, karibu na mpaka
unaotenganisha na wilaya ya Magu iliyoko
mkoani Mwanza.

“Tunaomba sana ndugu mwandishi waambie Watanzania kuwa mengi wanayoyasikia kuhusu Gamboshi si kweli kabisa, tunawakaribisha wote
hapa waje kufanya biashara na sisi, waoleane na vijana wa Gamboshi k**a wafanyavyo katika vijiji vingine. Sisi ni binadamu wema,” alidai mkulima Malimi Kidimi.

Lakini si wananchi tu wanaogopa kufika hapo hata baadhi ya makampuni ya ununuzi wa pamba.

“Kampuni Billlchard, moja ya mawakala wa kilimo cha mkatabaka alishindwa kutuletea mbolea hapa na badala yake akaenda kuibwaga katika kituo cha Polisi Bariadi kwa kile ambacho wafanyakazi wake walidai ni kuhofia usalama
wao,” alidai afisa mtendaji na kulaumu watu.

Wanaoneza hofu hiyo kuwa ina athari kubwa kwa kijiji na watu wake.
Kwa mujibu wa afisa mtendaji si kweli kabisa kila mtu ajaye Gamboshi hupotea moja kwa moja, huuliwa au kugeuzwa nyoka au fisi k**a wengi wanavovumisha.

“Pigo tulilopata kutokana sifa mbaya
tuliyobambikiziwa haisemeki ila ni madhara
makubwa tunayapata kutokana na kutengwa na jamii. Wanakijiji wa Gamboshi ni masikini kwa sababu mkondo wa maendeleo na mageuzi umepita mbali sana nao,” alidai mtendaji huyo.

Akifafanua kiini cha chuki na hofu waliyonanayo wananchi juu ya kijiji cha Gamboshi, afisa mtendaji huyo alidai kuwa

"hapo zamani ilitokea
kijana mmoja kutoka kijiji jirani cha Ngasamwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mzaliwa wa Gamboshi. Siku moja kijana huyo alikuja kijijini hapo akimsandikiza mpenziwe na kisha kushindwa kurudi kijijini mwake. Juhudi za kumsaka kijina huyo hazikuweza kuzaa matunda hadi aliponekana kichakani baada ya siku saba huku ngozi yake imebadilika na kuwa nyeupe.
Alipouliza alifikaje kichakani hapo, kijana huyo alijibu kuwa ameteremshwa na ndege ya JET kutoka Ulaya na baada ya hapo kijana huyo alirukwa na akili kiasi cha kushindwa kuuongea. Ilibidi achukuliwe na kupelekwa kutibiwa na waganga wa jadi na akapona baada ya matibabu ya zaidi ya mwezi mmoja,” alisimulia
afisa huyo, na kudai kuwa, kisa hicho
inawezekana kuwa na ukweli kidogo sana, lakini kuongezwa chumvi nyingi kupita kiasi.

Kwa mujibu wa Maduhu, tangu siku hiyo
Gamboshi ikatangazwa uadui na vijiji vingine kiasi cha kukifanya kuogopwa na kuchukiwa mno.

“Uvumi k**a Gamboshi inaweza kuonekana k**a Ulaya au Marekani ilianzia hapo na umendelea kurudiwa kwa namna ambayo imekifanya kijiji hiki kiitwe jiji la maajabu,” alidai afisa huyo.

Kwa maoni ya Malimi Kidima, Wana Gamboshi wangeweza kuitangazia dunia kuwa wao ni wasafi lakini, kwa miaka mingi wamekosa jinsi ya kuifanya sauti yao isikike.

“Redio ndiyo njia ya pekee inayotufanya sisi tuwe karibu na dunia. Hakuna mwenye luninga hapa kwa sababu hakuna umeme. Tunasoma magezeti kupitia vichwa vya habari vinavyosomwa kila siku redioni,” alidai Maduhu.

UKURASA HUU KWA HABARI MAKINI ZAIDI

Marapa wale wanakimbia
29/06/2021

Marapa wale wanakimbia

The man from konde gang go by the name killy
12/06/2021

The man from konde gang go by the name killy

01/06/2021

Address

Chanika
Dar Es Salaam
255

Telephone

+255682420365

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when B DADI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to B DADI:

Share