04/08/2025
KUTOKA KULA CHAI NA KAROTI MPAKA UDIWANI.
Nataka niseme jambo moja kwa ajili ya vijana wa Arusha na sio kwa ajili ya
Dogo Janja amekulia maisha ya hali duni, alizungukwa na kila aina ya beto, alipishana na mapusha wengi Ngarenaro kuliko alivyopishana na pengine na viongozi wa dini.
Ilikuwa rahisi kwa Dogo Janja kupata jani la bangi au miraa kuliko Mchicha. Nafikiri hakuna uhuni ambao Dogo Janja hakuzungukwa nayo.
Lakini alifanikiwa kuishinda hii vita.
Siku hizi kwenye vyombo vya habari Arusha utakutana na story za kutisha na aibu. Vijana wengi wanapoteza maisha kwa ulevi, uhuni, maradhi na uhalifu.
Mimi nimekulia Longdon, Arusha kata ya Sokoni One, enzi mimi nakuwa tulikuwa na vijana wengi wenye vipaji. Ulikuwa ukienda pale uwanja wa Sinoni ni balaa. Vijana wengi walikuwa na vipaji vya soka. Timu ya Kaka Majira ya Nyota FC na Young Life ni mashahidi.
Miaka ya nyuma tulizalisha wasanii wakubwa, River Camp ya akina , Nako 2 Nako , X-plasters, akina JCB, Chindo nk. Je tujiulize ndani ya miaka 10 Arusha imezalisha mastaa wangapi kimziki? Tuna timu ngapi za ligi kuu? Tumezalisha mastaa wangapi katika soka?
Kinachotrend kwa sasa Arusha ni nini? Ni WADUDU. Okay ubunifu huu wa WADUDU umezalisha vipi ajira kwa vijana? Iko wapi SUA iliyozalisha akina PACHA THE GREAT akina ?
Iko wapi ARACHUGA?
Siku hizi nikienda nyumbani Longdon vijana wameathirika na ulevi, gongo, bangi na mihadarati mingine. Unajiuliza kwanini mtoto wa miaka 19 tayari sura yake na maisha yake yameishi miaka zaidi ya 80?? Wamechoka.
Utasikia mara wamechomana visu kwa sababu alikuwa anamdai gongo ya mia tano, mara huyu kachomwa na wananchi kwa wizi. Iko wapi ARACHUGA?
Vijana Arusha wana mengi ya kujifunza kwa sitaki wajifunze kwa akina Nikki wa Pili au Joh Makini, nataka wajifunze kwa dogo mwenzao
Inawezekana mtu k**a amefika mbali sana ni ngumu kumtazama, je hata Dogo Janja aliyekuwa akiparua samaki na kuosha Karoti Kilombero hatumuoni?
Natamani kuona akipiga hatua kwenye nia aliyonuia pengine inaweza kwenda kuwaamsha vijana wa Arusha waliokata tamaa
Kaka SALAM