Jarida

Jarida > “Mind-blowing facts & stories daily �
Watch till the end �
� Join millions discovering the unbelievable”
SUBSCRIBE YOUTUBE�
(3)

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amefanya ziara katika eneo la makumbusho ya Hay...
14/04/2026

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amefanya ziara katika eneo la makumbusho ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere yaliyopo Mwitongo, Butiama mkoani Mara na kuwataka watanzania kumuenzi Kiongozi huyo kwa kuendelea kulipa Kodi kwa hiari.

Akizungumza wakati wa ziara yake Aprili 14, 2026 ikiwa ni siku moja baada ya siku ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Kamishna Mkuu Mwenda amesema enzi za uhai wake Mwl. Nyerere alikuwa akihimiza sana ulioaji wa kodi ili kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi.

Amesema lengo la ziara yake Butiama ni kwenda kushukuru kwa misingi ambayo Mwl. Nyerere aliiweka katika masuala ya kodi kwa kuhimiza kila mtanzania aliyetakiwa kulipa kodi analipa na kodi hiyo inakusanywa kwa uadilifu na kurudi kwa watanzania kwa kupitia miradi ya maendeleo ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema msingi uliowekwa na Baba wa Taifa umeendelea kuenziwa hadi hivi sasa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusimamia ukusanyaji wa kodi kwa kutoa miongozo kwa TRA ili kuiwezesha Tanzania kujitegemea kwa kikasi kikubwa kiuchumi.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuwakaribu na Walipakodi, kuwasikiliza, kutatua changamoto zao, kuwezesha biashara zao.

Katika ziara hiyo Kamishna Mkuu Mwenda ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa ikiwa ni sehemu ya kumuenzi

Wananchi wa Iramba Mkoani Singida wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa...
10/04/2026

Wananchi wa Iramba Mkoani Singida wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni sita kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja la Nkonkilanga, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira yake ya kujenga miundombinu ya usafiri na usafirishaji ili kukuza uchumi Vijijini, kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii pamoja na kuimarisha ustawi wa jamii.

Kulingana na wananchi wanufaika wa daraja hilo, wameeleza namna ambavyo walikuwa wakipata changamoto wakati wa msimu wa masika kutokana na mawasiliano kati Wilaya za Iramba, Mkalama na Kishapu kukatika, suala ambalo lilidhorotesha biashara, shughuli za kilimo na upatikanaji wa huduma muhimu, wananchi wakilazimika kukodi watu kwaajili ya kuvusha wagonjwa kwa kuwabeba kwa mikono ili kuwavusha kuelekea upande wa pili wa mto huo.

"Tulikuwa tunapata shida sana ila tunashukuru sasa hivi tunateleza tu bila shida ila mwanzoni tulikuwa tunahangaika sana kwani barabara ilikuwa inatuulia magari ila sasa hivi tunafanya kazi bila hofu na mawasiliano yapo muda wote hata wakati wa masika, kwakweli tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutukumbuka na kutujengea daraja hili." Amesema Rashid Nassoro, Dereva wa gari la mizigo.

Wananchi hao kadhalika wameishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kutatua changamoto hiyo waliyokuwa nayo kwa muda mrefu, huku Bw. Makonda Nkinga akibainisha namna ambavyo shughuli zao za Kilimo zimeimarika na hivyo kuongeza pato na uhakika wa soko hata wakati wa msimu wa masika tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ntwike Mhe. Ramadhan Kitulo na Bi. Halima Maswi, Mkazi wa Kijiji cha Nkonkilanga wameeleza furaha yao na hali ilivyokuwa awali kabla ya ujenzi wa daraja hilo, wakimshukuru pia Rais Samia pamoja na kumuombea afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi.

https://vt.tiktok.com/ZSHQx67Dx/

Wanachama wa Vikundi vya Vijana, wanawake na Watu wenye ulemavu Manispaa ya Singida Mkoani Singida, wamemshukuru Rais wa...
09/04/2026

Wanachama wa Vikundi vya Vijana, wanawake na Watu wenye ulemavu Manispaa ya Singida Mkoani Singida, wamemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kutoa Jumla ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia sita na nane ili kuwezesha Vikundi zaidi ya 116 kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi katika Mkoa huo.

Wakizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Aprili 09, 2026, Vijana hao kutoka kwenye Vikundi vya Salvation kinachojishughulisha na Kilimo cha kisasa cha vitalu nyumba na kikundi cha Florida kinachozalisha bidhaa za aluminium na vyuma, wameeleza kuwa fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha mwaka 2024/26, wakikiri kuzisubiri kwa muda mrefu kabla ya ndoto yao kutimizwa na Rais Dkt. Samia.

"Sisi k**a kikundi tunamshukuru sana Mhe. Rais kwani hii fursa tuliitamani sana kuipata kwa muda mrefu na sasa tumeipata tukiamini kuwa tutapata mafanikio zaidi na mpango wetu sasa ni kuzalisha mazao mengi zaidi. Kupitia mkopo huu nimenufaika pia binafsi kwani sikuwa na mradi wowote ninaousimamia na hata kilimo nilichokuwa nakifanya hakikuwa kikubwa hivi lakini kupitia mradi huu ninaamini nitapata faida kwa haraka" Amesema Ayoub Jumanne, Mwanakikundi wa Salvation Group.

Kulingana na Bi. Doreen Focus, Afisa Mikopo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida, amesema vikundi hivyo viwili miongoni mwa Vikundi 116 vilipata Shilingi Milioni 30 kila kimoja na kusema wamekuwa wakivisimamia kwa ukaribu ili kuhakikisha vinapata tija katika shughuli zao ili kuhakikisha vinakuwa na uwezo wa kurejesha mikopo yao kulingana na mikataba waliyokubaliana.

Kwa upande wake Bw. Mohamed Said kutoka kikundi cha Florida amesema mkopo wa Milioni 30 katika kikundi chao umewakwamua dhidi ya lindi la umaskini walilokuwa nalo hapo awali kwani mkopo huo umewaongezea kuaminika na kupata tenda kubwa zaidi ikiwemo tenda za utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kwaajili ya matumizi kwenye majengo na ofisi za umma.

Serikali ya Rais Dkt. Samia imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mikopo hiyo kwa lengo la kuimarisha shughuli zinazowaingizia kipato Vijana, wanawake na wenye ulemavu, msisitizo wa Rais Samia ukiwa ni kuhakikisha mikopo hiyo inafika na kueleweka kikamilifu kwa walengwa kwa kurahisisha upatikanaji wake pamoja na kuboresha ufanisi wa mifuko hiyo na kukuza uelewa kuhusu sifa na masharti ya kuweza kupata mikopo hiyo.

https://x.com/jaridatv/status/2042131849380606032?s=46

07/04/2026

Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi ya Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania - TAHLISO Ndugu Geofrey Kiliba, ametoa ufafanuzi juu ya hali ya uchumi nchini, akibainisha kuwa kupanda kwa bei ya mafuta na gharama za maisha si tatizo la Tanzania pekee, bali ni changamoto inayoyakabili mataifa yote duniani kwa sasa.

Akihojiwa na moja ya chombo Cha Habari Jijini Dar es Salaam Kiliba amesema kuwa hali hiyo ni nzito na haiwezi kumfurahisha mtu yeyote, bila kujali nafasi yake katika jamii, kwani athari za ongezeko la bei ya mafuta hugusa moja kwa moja mnyororo wa uchumi na maisha ya kila siku ya mwananchi.

"Sio tu kupanda kwa bei ya mafuta, upandaji wa gharama za maisha hakuna mtu yoyote anayeweza kufurahishwa... jambo hili ni la dunia kwa ujumla," amesema Kiliba.

Aidha, Kiliba ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania imeanza mapema kutafuta suluhu ya changamoto hiyo hata kabla ya mvutano wa Mashariki ya Kati haujaongezeka.

Amebainisha kuwa hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa, ikiwemo uwekezaji katika miundombinu ya uhifadhi wa mafuta, ambapo maghala yaliyopo kwa sasa yana uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa takribani siku 15.

"Serikali imeanza kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji na kupanda kwa bei ya mafuta... uwekezaji wa matanki ya kuhifadhi mafuta utasaidia kupunguza utegemezi wa uagizaji wa mara kwa mara," ameongeza.

Pia amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya gesi asilia, hasa katika sekta ya viwanda na taasisi za umma, ili kupunguza utegemezi wa mafuta na kukabiliana na mabadiliko ya bei duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka minne madarakani am...
03/04/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka minne madarakani ameiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuwa na Hospitali ya Wilaya kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 suala ambalo limepokelewa kwa furaha na wananchi wa Wilaya hiyo, wakiishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma za matibabu ya kibingwa karibu na makazi yao.

Wakizungumza na Mwandishi wetu wa habari leo Ijumaa Aprili 03, 2026, wananchi hao wameeleza kuwa awali kabla ya kujengwa kwa Hospitali hiyo iliyogharimu zaidi ya Bilioni tatu na Milioni 500, wananchi hao walilazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama kubwa kufuata huduma za afya, huku pia wakilazimika kuhifadhi miili ya wapendwa wao umbali mrefu kutokana na kukosa huduma za mochwari katika Wilaya hiyo.

Chini ya serikali ya Rais Samia, Uwekezaji mkubwa umefanyika Wilayani humo ambapo Imejengwa Hospitali hiyo yenye majengo 18 ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje OPD, jengo la wagonjwa wa dharura, jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la upasuaji, jengo la wodi kwa wanaofanyiwa upasuaji, Bohari ya dawa, Jengo la Mama na mtoto, wodi ya wanaume na wanawake, wodi ya watoto pamoja na jengo la kuchomea taka na mochwari.

"Kikubwa katika idara yetu ya Mama na mtoto tunaishukuru serikali kwa uwekezaji wake mkubwa sana na sasa tuna idara iliyokamilika kwa Vifaa vingi vya kumsaidia mzazi na mtoto mchanga katika hali zote za kujifungua kwa Mama kwa njia za upasuaji na kawaida na kwa watoto wanaozaliwa njiti tuma vifaa vya kuwatunzia na ICU ya watoto na zaidi tupo watumishi wa kutosha katika idara hii." Amesema Dkt. Giavila Albert.

Kwa upande wao wananchi ambao ni wanufaika wa Hospitali hiyo wamemshukuru Rais Dkt. Samia kwa huduma nzuri wanazozipata Hospitalini hapo, wakieleza kuwa kujengwa kwa Hospitali hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia ya kuendeleza na kudumisha utu wa Mtanzania kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki na kwa wakati sambamba na mpango wake wa kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa kusogeza huduma za matibabu karibu zaidi na wananchi

https://x.com/jaridatv/status/2040058001281736826?s=46

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeweka rekodi mpya kwa kukusanya shilingi trilioni 3.58 katika mwezi wa Machi 2026 pek...
02/04/2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeweka rekodi mpya kwa kukusanya shilingi trilioni 3.58 katika mwezi wa Machi 2026 pekee, ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 107.6 ya lengo lililowekwa.

Mafanikio hayo yameiwezesha TRA kukamilisha robo ya tatu ya mwaka wa fedha (Januari hadi Machi 2026) kwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 9.31, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.6 ikilinganishwa na kipindi k**a hicho mwaka uliopita.

Ufanisi huo umetokana na maboresho makubwa ya mifumo ya TEHAMA, hususan kuanza kutumika kwa mfumo mpya jumuishi wa kodi za ndani (IDRAS) mwezi Februari 2026, uliowezesha kusajili walipakodi wapya zaidi ya 69,000 pamoja na kuunganishwa kwa taasisi 92.

Aidha, kuimarika kwa mfumo wa forodha wa TANCIS kumechangia kuharakisha uondoshaji wa mizigo na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato katika vituo vyote vya forodha nchini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mafanikio hayo yanatokana na utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhimiza ulipaji kodi wa hiari kupitia ujenzi wa mahusiano mazuri kati ya TRA na walipakodi.

Kwa sasa, TRA imefanikiwa kuvuka malengo yake kwa miezi 21 mfululizo tangu Julai 2024, hali inayoashiria kuimarika kwa nidhamu ya ulipaji kodi pamoja na mazingira ya biashara nchini.

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuongeza uwajibikaji, ubunifu ...
01/04/2026

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuongeza uwajibikaji, ubunifu na weledi katika kutekeleza majukumu yao ili kuimarisha ukuaji wa sekta ya maziwa nchini.

Ameyasema hayo Aprili 01, 2026 wakati wa kikao kazi cha watumishi wa Bodi kinachoendelea katika Ukumbi wa Chuo Cha Kilimo Sokoine (SUA), mkoani Morogoro, Prof. Msalya alisisitiza umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti inayotekelezeka kwa vitendo, akieleza kuwa sekta ya maziwa ina nafasi kubwa katika kuboresha lishe, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Alibainisha kuwa ili kufikia malengo ya Bodi, watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, kuzingatia maadili ya kazi na kuwa wabunifu katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo, hususani katika maeneo ya uzalishaji, ukusanyaji na usindikaji wa maziwa.

Aidha, alieleza kuwa Bodi itaendelea kuimarisha usimamizi wa ubora wa maziwa pamoja na kurasimisha shughuli za wadau ili kuongeza ushindani wa bidhaa za maziwa za Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.

Akizungumza kandokando ya kikao kazi cha watumishi, Mteknolojia wa Chakula Bi. Christabel Swai, alisema kuwa kupitia mijadala na mawazo ya pamoja ya watumishi, Bodi itaweza kubuni mikakati bunifu itakayoboresha utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika kuleta mageuzi chanya kwenye sekta ya maziwa.

Naye Afisa Masoko Mwandamizi Bw. Hamis Kiimbi, alisema kuwa matarajio ya kikao hicho kitaibua mikakati thabiti ya kukuza masoko ya maziwa na bidhaa zake ndani na nje ya nchi na kuona ongezeko la uelewa kwa walaji kuhusu umuhimu wa matumizi ya maziwa, pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya masoko itakayowawezesha wafugaji na wadau wengine kupata masoko yenye tija zaidi, hivyo kuongeza kipato na kuchochea ukuaji wa sekta ya maziwa nchini.

Kikao kazi hicho cha siku mbili kinalenga kupitia na kujadili Mpango Mkakati wa Bodi wa miaka mitano ijayo, huku kikitarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa kuifanya sekta ya maziwa kuwa ya kisasa, yenye tija na inayochangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Wakulima wa Mpunga wanaofanya shughuli zao katika Bonde la Bahi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma wana...
01/04/2026

Wakulima wa Mpunga wanaofanya shughuli zao katika Bonde la Bahi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma wanatajwa kunufaika na uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shilingi Bilioni 3.6, zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya ukarabati wa skimu za umwagiliaji ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Samia wa kukuza na kuongeza uzalishaji na fursa za kilimo nchini.

Kulingana na Fundi sanifu wa umwagiliaji anayesimamia ukarabati huo Bw. Eliud Jeremia, amemueleza mwandishi wetu wa habari leo Jumatano Aprili Mosi, 2026 kuwa Mkandarasi tayari ameanza ukarabati huo, mradi ukitarajiwa kukamilika baadae mwaka huu na ukitarajiwa kuondoa changamoto ya uzalishaji duni wa zao la mpunga katika bonde hilo pamoja na kutoa hakikisho la maji kwa wakulima hao kwaajili ya umwagiliaji.

Wakieleza furaha yao na kumshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka na kuamua kutekeleza mradi huo katika eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 3,000 na likijumuisha wakulima zaidi ya 2,700, wakulima wanaotarajiwa kunufaika na ukarabati wa skimu hizo sita, wameeleza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo hapo awali ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za uzalishaji, suala ambalo lilisababisha faida kidogo pale wanapofikisha zao hilo sokoni.

"Ni muda mrefu tumekuwa tukilima zao hili la mpunga hapa Bahi katikati ya changamoto kubwa ya miundombinu mibovu iliyokuwa ikidhohofisha uzalishaji wetu lakini Mhe. Rais ametupatia fedha za ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji shilingi Bilioni 3.66 suala ambali litaongeza tija ya uzalishaji na kubadilisha kabisa uchumi wetu." Amesema Bw. Ramadhani Issa.

Wakati wa kampeni zake za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi kuendeleza mapinduzi ya kilimo kote nchini kwa kutoa ruzuku za mbolea na pembejeo, kujenga skimu zaidi ya 738 za umwagiliaji na kuimarisha zana za kisasa ikiwemo matrekta, Ahadi zake zikilenga kuongeza uzalishaji, kutanua wigo wa masoko ya mazao ya kilimo pamoja na kuwawezesha vijana kuingia kwenye kilimo kupitia programu ya BBT (Jenga Kesho Iliyo bora).

https://x.com/jaridatv/status/2039334144371511301?s=46

Jumla ya Shilingi Bilioni 14 za Kitanzania zimetolewa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza mradi wa ujenzi...
30/03/2026

Jumla ya Shilingi Bilioni 14 za Kitanzania zimetolewa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza mradi wa ujenzi wa Daraja la Nzali, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na kuondoa adha ya kukatika kwa mawasiliano pamoja na mafuriko kwa wananchi wa Vijiji viwili vya Nzali na Mahama.

Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo na kuanza kutumika kwa daraja hilo, wananchi wa Vijiji hivyo pamoja na maeneo mengine ya Chamwino wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja hilo, wakieleza kwamba daraja hilo pia limesisimua uchumi wa wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wa Vijiji hivyo na maeneo jirani kutokana na uhakika wa sasa wa usafiri katika misimu yote ya mwaka ndani ya Wilaya hiyo.

"Hata gari za wagonjwa zinaweza kuja kutoka upande wa pili, linafika hapa linashindwa kuvuka, kuna wakati mwingine wagonjwa walikuwa wanafia hapahapa kutokana na kushindwa kuvuka kupata huduma za matibabu upande wa pili kwenye Hospitali." Amesema Bw. Adam Mwangalimi, Mkazi wa Kijiji cha Nzali.

Kwa upande wake Bi. Baraka Sudai ameeleza kuwa kukamilika na kuanza kutumika kwa daraja hilo kumetimiza dhamira ya Rais Samia ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa wanawake kwani sasa wananchi wa Vijiji hivyo wanaweza kufika kwa uhakika na uharaka zaidi katika Vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa ujauzito.

""Nasema kabisa Mama Samia ni Mama wa watu, anayekubalika na ametusaidia vya kutosha katika Kata yetu, Wilaya na Taifa kwa ujumla ameonesha kazi kubwa sana iliyofanyika." Amesema Bw. Yohana Jackson Mkazi wa Nzali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kupeleka miradi ya ujenzi wa miundombinu katika maeneo ya pembezoni mwa Wilaya hiyo, akisema daraja hilo limekuwa muhimu katika kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii katika Wilaya hiyo ya Chamwino.

https://x.com/jaridatv/status/2038623452878234065?s=46

27/03/2026

Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Charles Odero amesema serikali na Vyama vyote vya siasa ni wadau muhimu katika mchakato wa maridhiano ulioasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa hakuna chama kikubwa cha siasa chenye sifa za ziada za kuhodhi mchakato huo k**a ambavyo baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikidhani vina nguvu zaidi ya kuhodhi mchakato huo kuliko vyama Vingine nchini.

Odero amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum aliyoyafanya leo Alhamisi Machi 26, 2026 kwenye kipindi cha Runinga Mtandaoni cha Front Page, akiwataka wanasiasa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo kwa kujifunza na kupata uzoefu kutoka kwa mataifa mengine yaliyopitia mchakato huo.

Akisisitiza kutungwa kwa sheria maalum ya kuendesha mchakato huo, Odero amewakosoa pia wale wote wanaodai kuwa hawaitambui serikali iliyopo madarakani pamoja na Bunge la sasa, akitaka wanasiasa na Vyama vya siasa kuheshimu serikali na Mihimili mingine ya nchi kwani imewekwa na wananchi licha ya kuwa Bunge lina asilimia kubwa ya viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi.

"Tusugue vichwa namna gani tutafanya haya maridhiano, binafsi natamani mchakato huu utanguliwe na sheria ya maridhiano ya Kitaifa Bungeni ili maridhiano haya yatambuliwe na sheria na baadae tuende kwenye utekelezaji wake na nialike Viongozi wa Vyama vya siasa tuangalie mazungumzo yetu yaweje badala ya kuanza kusema mtu hamtambui Rais, halitambui Bunge, k**a binadamu lazima tupate suluhu kwani hakuna asiyejua kuwa Dodoma kuna Bunge na Rais wetu ni Samia Suluhu Hassan." Amesema Wakili Odero.

Odero anaungana na Viongozi wengine wa siasa nchini wanaopendekeza ushiriki wa pamoja katika mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza umuhimu wa Vyama vya siasa kuwa sehemu ya maridhiano hayo badala ya namna ambavyo baadhi yao sasa wanataka kuwa vikwazo katika kufanikisha mchakato huo muhimu katika kukuza umoja wa Kitaifa, kuponya baadhi ya kasoro sambamba na kutafuta suluhu ya kudumu katika changamoto zinazoyakwaza makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii nchini.

26/03/2026

Ndoto za vijana zimeanza kudhihirika kwa vitendo baada ya kikundi cha “Vijana Ujenzi Workshop Yard” kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kunufaika na mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya shilingi milioni 80 inayotolewa na serikali chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan.

Kupitia mkopo huo, vijana hao wamefanikiwa kukuza shughuli zao za uzalishaji na kuimarisha hali zao za kiuchumi. Mafanikio hayo yamewawezesha si tu kujikwamua binafsi, bali pia kurejesha kwa jamii kwa kutoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule za eneo hilo, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Benton Albert, amesema mkopo huo umeleta mabadiliko makubwa kwa wanachama, wengi wao wakifanikiwa kujitegemea kiuchumi, kumiliki mali na kuendeleza biashara zao.
"Sisi kikundi chetu cha Vijana Ujenzi workshop Yard tulinufaika tukapata mkopo wa milioni 80, ambapo kwenye mkopo huo mpaka sasa tumesharejesha milioni 73.4 na tumenufaika kwa mkopo huo ambapo vijana wengi wameweza kujikwamua kiuchumi, wameweza kuendesha maisha yao na kupata vitu mbalimbali. Baadhi ya vijana hapa wamefanikiwa kupata viwanja, nyumba na biashara ikawa imesimama vizuri" Benton Albert, Mwenyekiti Vijana Ujenzi Workshop Yard

Aidha, mnufaika wa kikundi hicho, Joshua Nyaulingo, amesema mkopo huo umewapa dira mpya ya maisha na kuwafanya vijana wengi kuacha utegemezi.
"Kutokana na mkopo ambao tulipewa na Mheshimiwa Rais mimi nimekuwa mmojawapo wa mwajiriwa kwenye kikundi hiki na tumekuwa wanafaika kwasababu kupitia ule mkopo tumeweza kujikimu kimaisha pia tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa mkopo ule kwasababu vijana wengi ambao tuko pale tulikuwa mwanzo hatuna dira ila baada ya kupata ule mkopo tumekuwa na mwelekeo" Joshua Nyaulingo, mnufaika Vijana Ujenzi Workshop Yard

Walimu wa eneo hilo wamepongeza hatua hiyo, wakisisitiza kuwa ni mfano bora kwa vikundi vingine vya vijana kurejesha shukrani kwa jamii kwa kutumia fursa wanazopatiwa.
"Kwanza tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwakua amewakumbuka vijana na kuwapa mikopo ambayo imewawezesha kukidhi mahitaji yao na kusonga mbele, lakini tunawaomba pia vijana wengine ambao wamepata mikopo k**a hivi wakumbuke kuleta shukrani kwa jamii k**a wenzao ambao wametufanyia msaada mkubwa k**a huu" Mwalimu

Address

Nairobi
22054

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jarida posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share