Ushairi Kisasa

Ushairi Kisasa Ukurasa huu unahusu utunzi wa mashairi mbalimbali...ya harusi,tamasha mbalimbali, shule,na hata chuo kikui...
(1)

Allahu Akbar
01/06/2026

Allahu Akbar

Sautiyo...Sautiyo kisikia,moyo unakwenda mbio,Simu naikwamilia,tuli ikwenye sikio,Raha ikinizidia,dm ninakwenda mbio,Sau...
28/05/2026

Sautiyo...
Sautiyo kisikia,moyo unakwenda mbio,
Simu naikwamilia,tuli ikwenye sikio,
Raha ikinizidia,dm ninakwenda mbio,
Sautiyo mai dia,ndilo langu seleleo.

Ndio langu seleleo,linipalo sepetuko,
Macheo kwangu machweo,haviniishi vituko,
K**a pambe hini ndio,ilo nijaza ridhiko,
Sautiyo mai dia,inanijaza ukwasi.

Inanijaza ukwasi,vina vyanitiririka,
Tena sinayo tetesi,weye ndiwe langu rika,
Njoo tukate fenesi,kwa mama ujapofika,
Sautiyo mai dia,yaniondoa wahaka.

Yaniondoa wahaka,na mbio kwenenda moyo,
Yaviziba na viraka,michubuko iishiyo,
Wala sinayo haraka,hapo hapo ndo kwamiyo,
Sautiyo mai dia,imenijaa moyoni.

Imenijaa moyoni,taratibu yanongoa,
Na garagara ndazini,kwa furaha soishia,
Umenijaa chembeni,naserereka sikia,
Sautiyo mai dia,ni tamati nakwambia,

Ni tamati nakwambia,sifa zako mwanamama,
Kwako mie meridhia,pasi hofu ninahema,
Hadi tama tamatia,mwenzio Shakita hema.
Sautiyo mai dia,ndio bembelezi tosha.

Malenga Wa Pwani
Mombasa
©27/5/2026
Alhamdhulillah
tu...sauti...

Subhannallah
24/05/2026

Subhannallah

Alhamdhulillah Rabbillalamin
24/05/2026

Alhamdhulillah Rabbillalamin

Mashallah
24/05/2026

Mashallah

Kwa Sheikh Juma Saed Juma – Nipo kwenye mfululizo wa ufanisi! Nimekuwa shabiki bora kwa miezi 13 mfululizo. 🎉Alhamdhulil...
23/05/2026

Kwa Sheikh Juma Saed Juma – Nipo kwenye mfululizo wa ufanisi! Nimekuwa shabiki bora kwa miezi 13 mfululizo. 🎉Alhamdhulillah

Kwa Moh'd Vijdk – Nipo kwenye mfululizo wa ufanisi! Nimekuwa shabiki bora kwa miezi 18 mfululizo. 🎉
22/05/2026

Kwa Moh'd Vijdk – Nipo kwenye mfululizo wa ufanisi! Nimekuwa shabiki bora kwa miezi 18 mfululizo. 🎉

Address

Sunlight
Mombasa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushairi Kisasa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Ushairi Kisasa:

Share