SAUTI YA BARA.

SAUTI YA BARA. Mashairi ya Elimu,Mapenzi,Ndoa,Motisha,Dini na Siasa. Maneno ya Bara, Hisia za Maisha. Lugha ya Bara yenye Uhondo.

23/07/2026

"Mwenye pupa hadiriki kula tamu kwani tamu kwake si tamu ila ni chanzo cha tamaa na matamanio." Dondoo za Sauti Ya Bara.

All Online

Mgurumo huo wake, wakuza na kulea,Angalia hao wake, wamenyooka tabia,Angalia nyumbani, kifika wanafurahia,Baba ni nguzo ...
03/06/2026

Mgurumo huo wake, wakuza na kulea,
Angalia hao wake, wamenyooka tabia,
Angalia nyumbani, kifika wanafurahia,
Baba ni nguzo kuu, kwa malezi ya hao wana.

Oneni hawa wa sasa, heshima meadimika,
Tena hulka yao hasa, utu wao meondoka,
Shuleni inawapasa, walimu kuungulika,
Baba ni nguzo kuu, kwa malezi ya hao wana.

Twajua wengi hawana, na ni kudura yake Mola,
Ombi letu ya kufana, kina baba kulola,
Na Wakanye hao wana, wasalie kutia fola,
Baba ni nguzo kuu, kwa malezi ya hao wana.

Tuwakanye, tukosoe, ikilazimu tuadhibu.

.
, Hisia za moyoni.
Sauti Ya Bara

22/03/2026

Je, wajua kuwa mbwa wa tajiri akiuma mwanaume maskini huyo mwanaume ndiye atalaumiwa kwa kusimama kwa njia wakati mbwa wa tajiri alikuwa akipita?

.

, hisia za Maisha.

CHUKI.Chuki nayo haifai, niliona akilonga,Kuhusu izo vurumai, hadi zikatoa mwanga,Karibu wao wanaswe, na mtego wa maafa....
25/02/2026

CHUKI.

Chuki nayo haifai, niliona akilonga,
Kuhusu izo vurumai, hadi zikatoa mwanga,
Karibu wao wanaswe, na mtego wa maafa.
Chuki ni hatari, huangamiza utu.

Akikuchukia huyo, fitina tupa mbali,
Hata akiatua moyo, usimpangie njama,
Ombea wake moyo, aubadilishe Maulana.
Chuki ni hatari, huangamiza utu.

, hisia za Maisha.
.
.

HEKAHEKA ZA VALENTINO.Ona vile anang'aa, mbalamwezi  kwelikweli,Hana hata mawaa, umbo la mwanamwali,Urembo unaovutia, Un...
14/02/2026

HEKAHEKA ZA VALENTINO.

Ona vile anang'aa, mbalamwezi kwelikweli,
Hana hata mawaa, umbo la mwanamwali,
Urembo unaovutia, Unanasa ja chambo,
Hekaheka za valentino, zazidi kuvumisha miji.

Leo kapewa maua, nadhani ya waridi,
wanasema anazingua, ila leo imebidi,
Furaha yaenea, wakitimiza ahadi,
Hekaheka za valentino, zazidi kuvumisha miji.

, hisia za maisha.

.

UCHACHU WA VALENTINO.Valentino imewadia, umesikia mtaani?Wameanza kujipodoa, wajitokeze njiani,Nawaona wameondoa, vizuiz...
13/02/2026

UCHACHU WA VALENTINO.

Valentino imewadia, umesikia mtaani?
Wameanza kujipodoa, wajitokeze njiani,
Nawaona wameondoa, vizuizi vya moyoni,
Uchachu wa Valentino, unaliza wengi wana.

Nunua au nikuache, ni semi za hiyo siku,
Wanazidi zao cheche, valentino ya ruzuku,
upendo nao siache, uondoe dukuduku,
Uchachu wa valentino, unaliza wengi wana.

CHUKI YA NINI?Niliona ukitembea, ukisonya kila kona,unaeneza umbea, eti hiki na kile sina,Kwani nini wanakupea, au ni si...
12/02/2026

CHUKI YA NINI?

Niliona ukitembea, ukisonya kila kona,
unaeneza umbea, eti hiki na kile sina,
Kwani nini wanakupea, au ni siha huna,
Chuki ni sumu, jikaze usiinywe.

Hata kule kazini, naona mnagombana,
Tena mko mbioni, kwa fitina kupingana,
Utafika ukingoni, chimbuko ni fitina,
Chuki ni sumu, jikaze usiinywe.

11/02/2026

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Beaty Samuel's, Jefferson Kameta, Gideon Mutie, Yvonne Nduku, Esther Esther, Josphat Maithya, Boniface Nthakyo, Damaris Matheka

UPWEKE WA MAISHA.Mali tutafutazo, ni nzuri maishani,Hata kwa vikwazo, utawahi kazini,Wengi hata kwa uozo, huingia riziki...
10/02/2026

UPWEKE WA MAISHA.

Mali tutafutazo, ni nzuri maishani,
Hata kwa vikwazo, utawahi kazini,
Wengi hata kwa uozo, huingia rizikini,
Upweke wa maisha, umeenea duniani.

Ukipata hizo hela, unavuma kila kona,
unakuwa shelabela, hupiti kina Fiona,
unatia yako fola, badaye wanakudona,
Upweke wa maisha, umeenea duniani.

, hisia za maisha.
.
.

CHUO CHA MAISHA.Tangu ulipozaliwa, ulionja tamu na shubiri,Maisha yamekuwa, kufuata zao amri,Fanya au utafanyiwa, ndio y...
09/02/2026

CHUO CHA MAISHA.

Tangu ulipozaliwa, ulionja tamu na shubiri,
Maisha yamekuwa, kufuata zao amri,
Fanya au utafanyiwa, ndio yao desturi,
Chuo cha maisha, hakina Chopii,

Niliona mwafulani, kaegesha Pajero,
Unajua huko shuleni, alipata zake ziro,
Ila huu wa maisha, hapati hata kero,
Chuo cha maisha, hakina Chopii.

, hisia za maisha.
.
.

Address

28
Makindu
90138

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SAUTI YA BARA. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to SAUTI YA BARA.:

Shortcuts

Share

Category