31/05/2026
ποΈβ¨ HERI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU β¨ποΈ
Leo tunaungana na Kanisa lote kusherehekea Utatu Mtakatifu β Mungu mmoja katika Nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tunamshukuru Mungu kwa upendo wake usio na mipaka, unaotuunganisha katika imani, matumaini na upendo. β€οΈ
K**a Kwaya ya Mtakatifu Cecelia Mitaboni, tunamtolea Mungu sifa na shukrani kwa kipawa cha huduma ya uimbaji. Tunaomba Utatu Mtakatifu uzidi kutuongoza, kutuimarisha katika umoja, na kutubariki tunapoendelea kulitukuza jina la Mungu kupitia nyimbo zetu. πΆπ