07/08/2026
Somo la Agosti 8, 2026 (Av 25, 5786).
KUZAMISHWA (NDANI YA MAJI), NJIA YA ELOHIM YA UBATIZO
Somo Kuu: Mathayo 3.
Fungu La Kukariri: Wakolosai 2:12
1. Ubatizo wa Yahshua, jinsi gani ulifanywa na ulifanywa na nani? Mathayo 3: 13-16.
2. Mtume Paulo anasema nini kuhusu aina ya ubatizo katika siku alizoishi? Wakolosai 2:12.
3. Baada ya Pauli na Sila kufunguliwa kwa miujiza kutoka gerezani, ni mtu gani muhimu na familia waliamini na kubatizwa? Matendo 16: 29-33.
4. Tunapaswa kuenendaje baada ya kubatizwa, au kuzikwa pamoja Naye katika ubatizo? Warumi 6: 4.
5. Tutamvaa aje Masihi? Wagalatia 3:27.
6. Je! Sisi ni kwa kuzamishwa katika maji tumebatizwa katika kifo cha Masihi? Warumi 6: 3-4.
7. Kwa nani, na kwa namna gani, towashi aliyeamini alibatizwa? Matendo 8:38.
8. Ni aina ngapi za ubatizo zilizopo? Waefeso 4: 5.
9. Je, kulikuwa na watu wengi walioamini na kubatizwa baada ya kusikia mahubiri ya Petro siku ya Pentekoste? Matendo 2:41.
10. Je, kulikuwa na wengine ambao waliamini na kubatizwa baada ya kusikia mahubiri ya Filipo juu ya ufalme wa Elohim na Yahshua Masihi? Matendo 8:12.
11. Kwa nini Yohana alibatiza huko Aenoni? Yohana 3:23.
Maelezo. Aya zilizo hapo juu zinathibitisha ukweli kwamba kuzamishwa ni njia
sahihi ya ubatizo. Ikiwa kunyunyizia mtu maji hutosha, kwa nini Yohana alitaka
maji mengi ya kubatiza? Kunyunyizia mtu maji ni makosa, na ni hali ya
kusikitisha sana ambayo wengi wamewadanganywa na mafundisho hayo na bado wanataka kuyashikilia. Hebu tuombe ili waweze kuona mwanga wa kweli na kukubali nuru ya kweli na kukubali mpango wa Elohim wa wokovu kwa ukamilifu wake.
📸 Courtesy Pst Joseph Rotich